Na Gift Mongi MATUKIODAIMA Moshi
Michezo ni furaha lakini pia michezo hukutanisha ndugu pamoja kwa lengo la ustawi katika jamii zetu ambapo ni muendelezo wa maisha ya kila siku. Kwa hali hiyo viongozi mbalimbali wamekuwa wakihamasisha michezo katika maeneo yao ya kiuongozi hususani mchezo wa mpira wa miguu kwani umeonekana kuwa na ushabiki mkubwa, Mashabiki hawa kwa pamoja huufanya mpira wa miguu kuwa na wafuasi wengi ambapo kwa pamoja huileta jamii kwa pamoja na faida zake katika jamii ni kubwa zaidi,
Katika kata ya Kirua Vunjo Kusini anapotokea mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Moshi Vijijini Yuvenail Shirima ameanzisha mashindano ya mpira wa miguu yanayofahamika kwa jina la 'Yuvecup'
Akizungumza kuhusu mashindano hayo mwenyekiti huyo amesema mashindano hayo yana lengo la kuleta vijana kwa pamoja na kuwa mpira ni sehemu ya ajira. 'Mpira ni furaha lakini mpira ni sehemu ya ajira na ndio maana nimenzisha mashindano haya lengo ni kuleta jamii kwa ukaribu zaidi anasema.
Anasema kupitia mchezo ataweza kuibua vipaji mbali mbali ambavyo vijana watakuwa navyo lakini pia kupitia michezo huenda ikapunguza matukio ya kiuhalifu katika jamii, Jones Mlay miongoni mwa kijana anayeshiriki katika mashindano hayo anasema michezo huleta jamii kwa pamoja lakini pia ni kuinuia vipaji vilivyojificha.
Kupitia michezo au mashindano kama haya tunaweza kuibua vipaji vilivyojificha na hii huenda ikawa ni sehemu ya fursa Kwa vijana kutambulika katika medani za kimchezo anasema.
Mwisho.
0 Comments