Header Ads Widget

MAAFISA UHAMIAJI KAKONKO MBARONI TUHUMA KIFO CHA ENOS ELIAS

 Kamanda wa polisi Filemon Makungu

Mfanyabiashara wa Katoro mkoa Geita Enos Elias Mwenyeji wa wilaya Kakonko ambaye anadaiwa kuuawa akiwa mikononi mwa maafisa uhamiaji wa wilaya Kakonko mkoani Kigoma

Na Fadhili Abdallah, Kigoma 

POLISI mkoani Kigoma imewakamata maafisa wanne wa idara ya uhamiaji mkoa Kigoma wakituhumiwa kuhusika na Mfanyabiashara wa Katoro mkoa Geita mwenyeji wa kijiji cha Ilabiro wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Enos Elias  aliyeuawa akiwa kwenye mikono ya maafisa uhamiaji wilaya ya Kakonko.


Taarifa kutoka chanzo cha kuamimika wilayani Kakonko kimeliambia gazeti hili kwamba maafisa hao walikamatwa Ijumaa jioni na kuanza kuchukuliwa maelezo kuhusu kuhusika kwao na jambo hilo.


Afisa Uhamiaji mkoa Kigoma, Novatus Dawson amethibitisha kukamatwa kwa maafisa uhamiaji hao Kakonko na kwamba suala hilo lipo milononi mwa polisi mkoa Kigoma.


Kamanda wa polisi mkoa Kigoma, Filemon Makungu amethibitisha kukamatwa kwa maafisa uhamiaji hao wa wilaya Kakonko na kwamba ni hatua za uchunguzi kujua ukweli wa kuhusika na kifo cha Enos Elias


Makungu alisema kuwa bado maafisa hao ni watuhumiwa na ukweli utathibitika baada ya kufanyiwa mahojiano hivyo kwa sasa hakuna taarifa zaidi za kuelezea jambo.


Sambamba na hilo Kamanda Makungu amekataa kutaja idadi ya maafisa waliokamatwa wala idadi yao kwa maelezo isije kuingilia hatua za uchunguzi na kutaka watu wote wanaotaka taarifa wasubiri uchunguzi ukamilike na taarifa kamili itatolewa.


Mfanyabiashara huyo inasadikiwa kuuawa Oktoba 29 mwaka huu baada ya kukamatwa na maafisa uhamiaji Oktoba 27 kwenye kizuizi cha Kiomoka wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma.


  baada ya kukamatwa Mfanyabiashara huyo  alilazwa kituo cha polisi Kaonko na tarehe 29 alichukuliwa na maafisa hao wa uhamiaji Kakonko  ambapo taarifa zake hazikupatikana  tena hadi polisi walipotoa taarifa kuwepo kwa mtu aliyezikwa akisadikiwa kuwa ni Mfanyabiashara huyo  wiki moja baadaye.


Akihutubia mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Kiganamo mjini Kasulu  Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe alisema kuwa jambo moja la kukamatwa kwa maafisa hao limetekelezwa lakini akataka kuwajibishwa kwa Mkuu wa wilaya Kakonko na idara ya uhamiaji kutoa fidia kwa familia ya marehemu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI