Na Fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar
Licha ya juhudi mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika kupambana na migogoro ya ardhi lakini imebainika wanawake wengi vijijini wamekuwa ni wahanga wa migogoro hiyo ambapo kesi nyingi zipo katika mabaraza na mahakama za mijini hasa kwenye maeneo ambayo hayajapimwa.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya haki za ardhi kwa wanawake nchini Tanzania 2023, Mkurugenzi wa Miliki Kuu Wizara ya ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dr Upendo Matotola amesema ardhi ndiyo rasilimali inayomilikiwa na wengi walio maskini, hata hivyo ardhi hiyo imekuwa ikimilikiwa ambao ni wafugaji na wakulima hujikuta ikiwa kwenye migogoro baina ya wenyeji au wawekezaji.
Amesema kuwa, kutokuwa elimu ya uelewa mzuri wa sheria na haki za watu katika kumiliki ardhi ni kikwazo kwa watu walio wengi katika kujiletea maendeleo, haswa kwa wanawake waishio vijijini na hatimae kushindwa kutumia rasilimali hii kwa manufaa makubwa ya kuinua uchumi wao.
"Maeneo mengi ya vijijini hapa nchini, ardhi ndio rasilimali inayomilikiwa na walio wengi ni maskini, hata hivyo ardhi hii ambayo imekuwa ikimilikiwa wengi ambao ni wafugaji, wakulima hujikita ikiwa kwenye migogoro baina ya wenyeji au wawekezaji"amesema Dr Matotola.
Aidha,amesema kuwa, Serikali kupitia wizara ya ardhi inawaahidi wananchi wote kushughulikia migogoro yote inayohusiana na ardhi na kuhakikisha inamaliza changamoto zote kwa haraka na kuhakikisha migogoro yote mikubwa kwa midogo inafanyiwa kazi ili kulinda amani na utulivu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Liberty Sparks Dr Samweli Alananga amesema utafiti huo uliozinduliwa umegusa maeneo mbalimbali ya Afrika ikiwemo nchi ya Tanzania na tumeangalia wapi kuna changamoto hasa katika umiliki wa ardhi ambayo ni rasilimali inayotoa ajira nyingi kwa wanawake vijana na kutoa suluhisho ili kusaidia kuleta uhuru wa kiuchumi na haki sawa kwa wote.
Aidha, amesema kuwa asilimia kubwa ya ardhi ya Afrika haijarasimishwa ambapo asilimia 10 tu, ndio imerasimishwa.
Naye, Mdau wa Maendeleo Elias Nawela amesema kuwa umiliki wa ardhi kiholela unasababisha migogoro mingi ya ardhi kuongezeka kwa makazi ya mijini na kupanuka kwa maeneo yanayokua kwa haraka na kuibua migogoro mipya.
0 Comments