Matukiodaima APP, Tandahimba
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Baisa Abdallah Baisa amekemea tabia ya watumishi wanaokuja katika halmashauri hiyo kuifanya kama daraja ambapo wakipata ukuu wa idara wanaondoka.
Kauli hiyo ameitoa jana katika baraza la madiwani ambapo alisema kuwa kumekuwa na tabia ya watumishi kufika katika wilaya hiyo wakiwa na mikakati ya kupata ukuu wa idara ambapo wakishapanda wanahama.
Amesema kuwa kitendo cha watumishi kutumia wilaya hiyo kama daraja kimekuwa kikisababisha kuwepo makaimu wengi.
“Wanakuja watumishi wakiwa sio wakuu wa idara wakifika wakipata ukuu wa idara wanahama hii kwa sasa hatutakubali yaani tunapandisha wanatumia kama njia hatuwezi kukubali tuna shida kwenye baadhi ya vitendo hata DMO tuliyenae ni kaimu mwaka wa pili hapandi” amesema Baisa.
0 Comments