Header Ads Widget

HALMASHAURI YA SIHA YAJIVUNIA MATUNDA YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA.

 



NA WILLIUM PAUL, MOSHI. 


HALMASHAURI ya wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro imepokea zaidi ya Bilioni 21.750 kwa ajili ya miradi mbali mbali ya maendeleo katika sekta za  Elimu, Afya, Kilimo, Mifugo na uwezeshaji wananchi kiuchumi na mfuko wa kaya maskini (Tasaf) . 


Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Dkt. Haji Mnasi wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha Machi 2021 hadi Oktoba 2023.



Dkt. Mnasi alisema kuwa, miradi iliyotekelezwa katika kipindi hicho ni ujenzi wa shule mpya za awali na msingi 6, shule mpya za sekondari 2 na kufanya halmashauri hiyo kuwa na jumla ya shule za msingi 70 na sekondari 17.


Alisema kuwa, miradi mingine iliyotekelezwa ni kituo cha Afya 1 na zahanati 4, hali ambayo imesaidia wanachi kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kufuata huduma za Afya na kupelekea kupunguza vifo. 



Aidha Mkurugenzi huyo alitumia nafasi hiyo kuishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hasani kwa kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi. 


Mwisho. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI