Header Ads Widget

DC HANIU AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

Mkuu wa wilaya ya Rungwe  Jaffar Haniu Jaffar Haniu   amefanya ziara na kukagua miradi ya Maendeleo katika maeneo mbalimbali.

Baadhi ya miradi aliyotembelea ni pamoja na  ujenzi  wa kituo kipya cha afya Kiwira na Masoko, Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha Lami katika mji wa Tukuyu na Ndulilo- Itete, shule mpya ya sekondari Lupepo na Isaka pamoja na Mradi wa maji Mabonde.


 Haniu amepongeza hatua ya ujenzi iliyofikiwa na kuwa kufanya hivyo itasaidia kufikia malengo mahususi ambayo Serikali imejiwekea kwa wananchi wake.



Haniu ameeleza kuwa Serikali kupitia Ilani ya Uchaguzi ya ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka  2000/25 imejipambanua wazi kuhakikisha watu wake wanafikiwa na huduma muhimu kama Barabara, Maji, Elimu na Afya.


Hivyo kwa hatua hii wakazi wa kijiji cha Ndulilo-Itete umbali wa KM 11.5 wanaenda kupata huduma ya barabara kwa kiwango cha Lami hatua itakayosaidia wakulima kusafirisha Mazao yao  kwa ufanisi Mkubwa.



Aidha Serikali imetoa kiasi cha shilingi Billion 1 Million 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha  Masoko na Kiwira hatua itayoimarisha afya za wakazi wa kata hizi.

Hata hivyo amepongeza hatua ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari Lupepo inayotarajia kugharimu kiasi cha shilingi  million  583.5 Fedha zilizotolewa na Serikali kupitia Mpango wa SEQUIP.

Shule hii yenye vyumba vya madarasa, Maabara, utawala, TEHAMA,  na Vyoo inatarajiwa kufunguliwa mapema januari 2024.

Nao wananchi wamepongeza kwa hatua nzuri ya serikali kuwaletea miradi ya maendeleo na kuahidi kuitunza kwa ajili ya kizazi hiki na kijacho.

Juma Mwasumbi Mkazi wa kijiji cha Itete ameshukuru kwa hatua ya ujenzi wa barabara ya lami kijijini kwao na kuwa itaharakisha maendeleo kwa wakazi wa kata hiyo.

Naye Aisha Asulwisye Mkazi wa kijiji cha Lupepo ameshukuru kwa ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika kata yao na kuhamasisha wazazi wote kupeleka watoto msimu ukiwadia ikiwemo uchangiaji wa chakula cha mchana kwa wanafunzi ili kuondoa Utapiamlo na kuongeza ufaulu wa masomo.


Pamoja na Pongezi hizo Mhe Haniu ameagiza mafundi wote wanaotekeleza miradi hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia Weledi, Ujuzi na Maarifa ili ikamilike kwa wakati na kutoa huduma kwa Wananchi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI