Na,Jusline Marco;Arusha
Waziri wa Maendeleo ya jamii,jinsia ,wanawake na makundi Maalum Dkt.Doroth Gwajima amesema kuwa serikali ya awamu ya sita imendelea kuweka katika wizara ya maendeleo ya jamii kwa kuandaa mpango wa Taifa wa kusimamia na kutekeleza maendeleo katika ngazi ya msingi.
Akizungumza katika maafali ya 13 na kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Chuo cha Maendeleobya Jamii Tengeru Dkt.Gwajima amesema mpango huo umejengeka katika falsafa ya wananchi ni kitovu cha maendeleo, ukiwa na madhumuni ya kuwezesha wananchi kushiriki maendeleo yao wenyewe kwa kutumia rasilimali walizonazo.
Aidha amesema utekelezaji wa mpango huo utawezesha wananchi kushiriki moja kwa moja katika shughuli za maendeleo ambapo ameuelekeza uongozi wa chuo cha maendeleo ya Jamii Tengeru kuhakikisha wataalamu wanaoandaliwa wanaufahamu mpango huo vizuri sambamba na kuandaa mafunzo kwa wanajamii ili kuwezesha utekelezaji wa haraka wapango huo.
Ameeleza kuwa tayari Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu ametengeneza mifumo, kazi iliyobaki ni kwa maafisa wa maendeleo ya jamii kuitekeleza mifumo hiyo kwa kuzifikia jamii zinazowazunguka na kutatua changamoto zao.
Ameongeza kuwa katika kuhitimisha shughuli za maadhimisho ya miaka 60 ya maendeleo ya jamii,ni fursa kwa Chuo kujitafakari kuhusu kuongeza mchango wake katika sekta ya maendeleo ya jamii kwa kuzingatia mabadiliko ya dunia kwa sasa katika kujikita kuwaandaa wahitimu wenye stadi na maarifa ya kukabiliana na soko la ajira nchini.
"Mafunzo mnayoyatoa yakawezeshe wahitimu kujiajiri na kutoa ajira kwa wengine ,wao wenyewe na wazione fursa na kuzalisha ajira zao na ajira za wengine kwa kuandaliwa vizuri na zana za uanagenzi na ubunifu wa kidigitali na kuskma fursa zilizopo."alisisitiza Waziri Dkt. Doroth Gwajima
Sambamba na hayo Dkt.Doroth amewataka wahitimu hao kuwa wabunifu,wajiamini na kuwa nyenzo zote muhimu za Tehama katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwa ni pamoja na uimarishwaji wa taaluma kwa kuzingatia Tehama na changamoto zinazoikabili dunia ya sasa ambapo amekitaka chuo hicho kufanya tafiti kubwa ili kuwasidia wananchi kubaini vikwazo na changamoto katika kujiletea maendeleo yao.
Amebainisha kuwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum inatambua mchango wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru na kupitia kurugenzi wataendelea kushirikiana ili kuona awamu inayofuata baada ya miaka 60 ni kwa namna gani itayashughulikia mambo mbalimbali waliyonayo.
Awali akizungumza katika Maafali hayo Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt.Bakari George amesema shehere za maafali hayo zinahitimisha kilele cha miaka 60 ya chuo hicho ambapo zilianza Mei 2023 na shughuli mbalimbali zilifanyika kuelekea siku ya kilele cha maadhimisho hayo ikiwemo utoji wa mfunzo kwa makundi ya jamii,warsha mifahalo na makongamano,maandalizi ya makala maalum ya miaka 60 ya chuo.
Dkt.Bakari amesema kwa kuzingatia kuongezeka kwa wanafunzi wanaoacha masomo kutokana na changamoto ya kutokuwa na uwezo wa kulipa ada na kumudu gharama za masomo, chuo kimeanzisha mfuko maalum wa udhamini ambao nijitihaha za chuo hicho katika kushawishi wadau mbalimbali kuchangia ili kuwezesha wanafunzi wenye changamoto hizo kuweza kukamilisha ndoto zao.
Ameongeza kuwa tangu kuanzishwa kwa chuo hicho, chuo kimepitia hatua mbalimbali za ukuaji ikiwemo mabadiliko ya kimuundo,kiutawala, kiutendaji na kitaaluma ambapo pia chuo hicho kinatarajia kuwa kitovu cha taaluma ya maendeleo ya jamii Tanzania na nchi za Kusini mwa jangwa la sahara ikiwa ni utekelezaji wa maono ya waasisi wa chuo hicho.
Pamoja na hayo Dkt.Bakari amesema kuwa mipango na mikakati ya chuo ni baada ya miaka 60 ni kuimarisha utekelezaji wa majukumu kwa kuweka uwiano sahihi katika nadharia na vitendo,kuweka mkazo madhubuti katika dhana za uanagenzi,ushirikishwaji wa jamii na ubunifu kwa kuzingatia ushirikishaji wa mifumo ya Tehama ili kupata matokeo ya haraka.
Ameongeza kuwa kupitia mpango mkakati wa chuo,chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru kimeweka malengo ya kuimarisha miundombinu ya kujifunzia na Tehama ili kuwavutia wanafunzi wa nje ya nchi ambapo katima mwaka wa fedha 2023/24 chuo kinatarajia kuanza ujenzi wa jengo la utawala la ghorofa 3 ambalo itaweza kutatua changamoto ya uhaba wa ofisi uliopo kutokana na kuongeza kwa watumishi hivyo kuchochea kuongezeka kwa tija mahali pa kazi.
Jumla ya wahitimu 1652 huku wanawake wakiwa 1077 sawa na asilimia 65.2 huku wanaume wakiwa 575 sawa na asilimia 34.8 ambapo wametunukiwa shahada ya Uzamili, shahada ya kwanza, Stashahada pamoja na Astashahada .
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Biashara Dkt.Ndalahwa Masanja amewataka wahitimu hao kuitumia elimu waliyoipata na ujuzi kulet mabadiliko chanya katika jamii ili wapate kuthaminiwa na kuwa wanyenyekevu,wenye kuheshimu watu wote na kujiheshimu na kuwa mfano wa kuigwa na jamii inayowazunguka.
0 Comments