Header Ads Widget

ARUSHA WOMEN IN BUSINESS WASISITIZA WATU KUPATA ELIMU YA FEDHA ILI KUKUZA UCHUMI WA FAMILIA.

NA NAMNYAKI KIVUYO, ARUSHA

Wito umetolewa kwa akina mama na watoto wao kujiunga na saccos ya wanawake mkoani Arusha  ili kuweza kupata elimu ya fedha itayosaidia kuendeza uchumi wa familia, jamii na taifa kwa ujumla.


Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa bodi ya chama cha ushirika cha  wanawake cha akiba na mikopo (Arusha women in business) Dkt Nsiande Urasa wakati akiongea na waandishi wa habari baada ya kushinda tuzo ya Saccos bora Tanzaniania  katika maadhimisho ya wiki ya huduma za fedha yaliyofanyika mkoani Arusha ambapo alisema kuwa mtu anaweza kuwa fursa na akawa na fedha lakini bila kuwa na elimu ya masuala ya fedha fedha ile inaweza kupotea.


“Chama chetu kinaamini kwamba ushirika ni biashara, pia tunaamini ushirika ni mahusiano na tunaamini mahisiano hayo wananachama wetu tunawapa zaidi wakati tunashiriki nao elimu ya fedha kwani biashara ni fursa na biashara ni fedha na mtu anaweza akawa na fursa, akawa na fedha ila  asipokuwa na elimu ya fedha, fedha ile inapotea, fursa inapotea na kupelekea biashara kufa,” Alisema Dkt Urassa.


Alifafanua kuwa Saccos hiyo ni Saccos ya akina mama wafanyabiashara na wajasiriamali wa jijini Arusha yenye uzoefu wa miaka 20 ambapo chama hicho kilianza kama wazo ikawa kikundi na baadae 2003 ikawa Saccos na wanaweka msingi na msisitizo mkubwa kwenye elimu ya Fedha na wanatarajia kufungua matawi  katika mkoa wa Kilimanjaro na Dodoma.

kwa upande wake Meneja wa chama hicho Maria Maembe alisema kuwa ni mafanikio ya tuzo waliyoipa ni kutokana na kufuata sheria za ushirika na kuwahamasisha wanawake waweze kujiunga kwenye vyama vya ushirika wa kutoa mikopo wenye riba nafuu, kuwafundisha elimu ya fedha na kuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba.


“Sisi Tunatoa huduma mbalimbali ikiwemo huduma ya akiba ambayo tunamfundisha mwanamke kujiwekea akiba kama tunavyoelewa baadhi ya wanawake hawako vizuri kwenye kutunza fedha, akipata hela kidogo atataka kununu Wigi, Viatu ,pochi yaani mwanamke mmoja anaweza anaweza akawa na pochi 200 lakini bado akaendelea kununua na kwa mwaka kati ya hizo anaweza akabeba kumi tuu na huo ni upotevu wa pesa kwahiyo tunawafundisha jinsi ya kuweka akiba,” Alisema.


Alifafanua kuwa katika akaunti yao ya akiba wana akiba ya aina tatu, akiba ya watoto ambayo wanawafundisha watoto wa wanachama kujiwekea akiba kwanzia wakiwa wadogo ili waweze kuwa na nidhamu ya fedha, wana akiba ya lazima ambayo hiyo mwanachama anaweka kila mwezi kiasi kisichopungua 20,000 lakini pia akiba ya kitega uchumi  na hiyo ni kwaajili ya watu  wenye mipango yao ya kimaisha kama vile kununua kiwanja, kununua Nyumba, Gari na mengineyo.


“ Napenda kuwaambia watanzania wajiunge kwenye vyama vya ushirika kwasababu hivi vyama vinasaidia sana, vinakutoa sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwani watapata elimu ya fedha, wataweka akiba kila mwezi na hawatakuwa na matumizi mabaya ya fedha, watapata mikopo mbalimbali  ambayo itawasaidia kuendeleza shughuli zao.


Hata hivyo Arusha women in business mpaka sasa imeshinda Tuzo 6 katika ngazi  ya saccos kitaifa na  ili mtu aweze kujiunga na chama hicho ni lazima awe mwanamke mwenye umri kwanzia miaka 18 kwenda juu, awe mkazi wa Arusha, awe mfanya biashara au mjasiriamali ikiwa ni pamoja na kuwa na utayari wa kufuata taratibu na sheria zinazoendesha vyama vya ushirika na utayari wa kujifunza uwekaji wa akiba kwa kujiwekea akiba kila mwezi lakini pia kuweza kununua hisa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI