Header Ads Widget

WANANCHI ACHENI KUFANYABIASHARA KANDO KANDO YA MAENEO YA RELI

 

Damas Mwajanga; Mkuu Wa Chuo Cha Teknolojia
Ya Reli Mkoani Tabora
akiwamwalisha mkurungezi mkuu wa TRC


Regina Tarimo; Afisa Uhusiano Mamlaka ya
Reli ya Tanzania-Zambia (
TAZARA)
akifafanua jambo na mbele ya
waandishi wa habari hawapo pichani.


Na Lucas Raphael,Tabora

 

 

Wakati nchi ya Tanzania ikiwa imeungana na mataifa  mengine ya Afrika  katika kuadhimisha wiki ya  usalama wa reli ,wananchi wametajwa  kuwa hatarini kuendelea kupoteza maisha kutokana na ubishi wa kufanya shughuli za kibinadamu  kwa kufanya biashara na kuweka vijiwe  vya kupiga soga na kupumzika   katika njia za reli.


Kauli hiyo imetolewa na Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania-Zambia Tazara, Regina Albert Tarimo alipokuwa akifanya mahojiano na Waandishi wa habari katika viwanja vya chuo cha Tektenolojia ya Reli Mkoani Tabora.

 

Alisema kwamba wananchi Kufanya biashara na mapumziko katika mazingira ya njia za reli ni makusudi ya kutekeleza ufunjifu wa sheria kwani kuna uwezekano mkubwa wa wananchi kugongwa na treni pengine hata  kusababisha ajali kufuatia uharibifu wa miundo mbinu unaotokana na shughuli zingine za kibinadamu.

 

“Kujenga  karibu na  njia ya reli ni hatari kubwa, kuna wananchi wamekuwa wakifanya shuguli zao za kibinadamu  hairuhusiwi  kuchunga mifugo pia hata kulima katika maeneo ya reli”


Alisema kwamba kutokana na hali hiyo wanaendelea kutoa elimu kupitia kampeni za usalama ambazo zitawasaidia wananchi kuweza kuepukana na ajali zinazotokana na uzembe .

 

Alisema kwamba elimu kupitia kampeni za usalama zitawasaidia wananchi kwa sababu suala la ajali limekuwa tatizo kutokana na kukatisha hovyo kwenye maungio ya reli na barabara.

 

“Changamoto kubwa ni suala la Usalama, hivyo wamekuja Mkoani hapa kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi na watumiaji wa vyombo vya moto kwa namna ya kuwa salama kwenye maeneo ya reli.

 

Mwakilishi wa mkurugenzi mkuu TRC na mkuu wa chuo cha  Tektenolojia ya Reli Mkoani Tabora Damas Mwajanga  alisema kwamba Shughuli za kibinadamu zifanyike nje  na maeneo ya  reli na kwa maeneo ya mjini  iwe umbali angalau wa mita 20 kutoka ukingo wa reli  na  nje.

 

Alisema kwamba kwa yale maeneo ya  halmashauri umbali isipungue mita 30 na kuwataka   wananchi  kuwa na  jukumu  la kulinda  miundo mbinu ya reli ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea mara ajali inapotokea.

 

“Ili kuhakikisha usafiri wa reli unakuwa salama na wenye tija  serikali ilitunga sheria  ya reli namba 10  ya mwaka 2017, sheria hiii imejikita katika usalama  na ulinzi wa miundombinu ya reli  na imeweka bayana kuwachukulia hatua kali watakaofanya hujuma ya miundo mbinu ya reli”.

 

Awali Akifungua maadhimisho ya wiki ya usalama wa reli  kitaifa yanayofanyika mkoani hapa Mkuu wa wilaya ya uyui  Zacharia Mwansasu kwa niaba ya  mkuu wa mkoa wa  Tabora balozi Dkt. Batilda Burian  alitilia mkazo suala zima la kumekuwepo na tatizo kubwa la kutumika vibaya kwa njia za reli  ikiwemo kugeuzwa kama sehemu za kupumzika, vijiwe vya kupiga stori, njia za kupita kufanyia biashara  pamoja na shughuli nyingine za kibinadamu kama kilimo sanjali na kuchungia wanyama.

 

Maadhimisho ya wiki ya usalama wa reli kitaifa yanaendelea  mkoani Tabora ambayo yanafanyika kwa muda wa siku tano  yakijumuisha mamlaka mbalimbali za usafirishaji. 



 

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI