Header Ads Widget

TPHPA SASA KUIMARISHA AFYA YA MIMEA KIDIGITALI, KANDA ZOTE KUNUFAIKA

NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA

Mamlaka ya afya ya mimea na viuatilifu Tanzania(TPHPA) imepokea vitendea kazi mbalimbali ikiwemo magari, ndege nyuki (drones), kopyuta,vishikwambi, mini lab na vinginevyo kutoka shirika la chakula na kilimo Duniani (FAO) kwa kushirikiana na umoja wa Ulaya (Eu) mradi wenye thamnai ya bilioni 2.2.



Akizungumza katika makabidhiano ya vifaa hivyo yaliyofanyika katika makao makuu ya mamlaka hiyo Ngaramtoni wilayani Arumeru mkoa wa Arusha  Naibu waziri wa kilimo David Silinde alisema kuwa,Serikali ya awamu ya Sita kufikia mwaka 2030 imeweka malengo  kuboresha na kuhakikisha ina jitosheleza kwa mahitaji ya chakula ndani na kuwa na ziada ya  kuuza nje ya nchi.


Alisema kuwa uzalishaji wa chakula 2021/2022 ulikuwa ni tani milioni 17.4 huku mahitqji yakiwa ni tani milioni 15.07 na ziada ikiwa ni tani milioni 2.3 ambapo kilimo huchangia mapato yatokanayo na mauzo ya nje kwa kiasi cha shilingi  dola za kimarekani bilioni 1.2 sawa asilimia 20 ya mauzo ya nje lwa mwaka.


“Serikali imeweka malengo kwa wizara ya kilimo mojawapo ni kujitoeheleza kwa mahitaji chakula ndani ya nchi na kuuza nje ya nchi ziada, kuongeza uwekezaji na kujenga na kuboresha miundo mbinu ya umwagiliaji ili kutumia fursa iliyopo ya hekta milioni 29 lakini pia kuongeza mazao ya kilimo kupitoa kilimo cha umwagiliaji kutoka asilimia 10 hadi kufikia asilimia 50,” Alisema Silinde.



Alifafanua kuwa uimarishwaji wa TPHPA ni moja ya vipaumbele vya wizara katika kuhakikisha malengo ya wizara katika kuhakikisha kuongeza mauzo ya nje  ya mazao kutoka bilioni 1.2 ya dola za kimarekani hadi kufikia dola bilioni 5 ambapo lengo hilo litatimia kupitia huduma bora za ukaguzi na udhibiti utakaofanywa na mamlaka hiyo.



Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania TPHPA Prof. Joseph Ndunguru alisema kuwa kupidia mradi huo (STEPHIT) wamepokea Magari aina ya Landcriser 7, Pikipiki 19, kompyuta 34, Drones20, Vishikwambi 41, Mini lab inspection tables 17, Friji 17, Wifi routes kwaajili ya internet17, esnet switch 17, ilumineted magnifire 17, vyenye thamani ya bilioni 2.2 fedha za kitanzania.


“Vifaa hivi vitaenda kuimarisha ofisi za kanda kwa kupeleka huduma zetu karibu ma wakulima ambapo vitatoa mchango mkubwa sana katika utekelezaji wa majukumu ya mamlaka ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa ufanisi katika shughuli za afya ya mimea na udhibiti wa viuatilifu , kuongezeka kwa uhakika wa chakula na malighafi za viwanda, ” Alieleza Pro Ndunguru.


“ Lakini pia tunategemea kupungua kwa uvamizi wa visumbufu vipya kutokana na kuimarika kwa uchunguzi kwa kupitia ndege nyuki hizi hali itayosaidia kuvidhibiti kabla havijaleta madhara kwa wakulima Mamlaka,” Alisema


 hiyo kwa kushirikiana na serikali imefanya uchambuzi wa sampuli za udongo 1300 kutoka kwenye mashamba pia Mamlaka imetoa mafunzo ya matumizi sahihi salama ya Viuatilifu kwa wakulima na maafisa ugani 1643 na wauzaji 631 wa Viuatilifu kutoka maeneo mbalimbali.



Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TPHPA Prof. Andrew Temu amesema kwamba uwekezaji Mkubwa ambao serikali inaweka kwenye sekta ya Kilimo unaopelekea wadau wa maendeleo wa kimataifa EU na FAO kuunga mkono juhudi za kuendeleza Kilimo nchini.


Alisema ufadhili wa Umoja wa ulaya kifedha na Shirika la maendeleo ya Kilimo Duniani  katika Mradi huu wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea kwa Lengo la kuhakikisha usalama wa chakula  unadhihirisha kukuza Kilimo endelevu na ulinzi wa mazingira kupitia mipango yake.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS