Header Ads Widget

TANZANIA YANG'ARA SEKTA UTALII, YAJIPANGA KUVUTIA ZAIDI WATALII

Na Fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar

Sekta ya Utalii nchini Tanzania yazidi kung'ara barani Afrika baada ya kujinyakulia tunzo 8 katika vipengele mbalimbali vya vivutio vya utalii na wadau wa huduma za utalii nchini humo, vilivyoshindanishwa na Mtandao wa World Travel Awards kuanzia Nov 17, 2022 hafi Mei 22, 2023.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Masoko wa TTB Dkt. Glastone Mlay amesema kuwa, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) inawajulisha umma kuwa mtandao wa WORLDT RAVEL AWARDS mwaka huu 2023 umetangaza washindi mbalimbali kwenye Mashindano yanayohusisha, Vivutio vya Tanzania, Bodi za nchi zinazosimamia Utalii, makampuni yanayojishughulisha na Utalii Afrika na Duniani kote katika nyanja mbalimbali.


Amesema kuwa, TTB mwaka huu imeibuka mshindi katika vivutio vya utalii na wadau wa huduma za Utalii nchini wameibuka washindi katika mashindano yaliyotangazwa katika hoteli ya “Atlantis the Royal” Dubai Oktoba 15, 2023.

 

“Mwaka 2023, TTB na Taasisi za wizara zilishirikiana na sekta binafsi kwenye kutangaza vivutio na hatimaye kupigiwa kura kwa ubora na vigezo vilivyowekwa na World Travel Awards kuanzia tarehe 17 Novemba,2022 hadi tarehe 22 Mei 2023,”.

 

Aidha, amefafanua vipengele ambavyo vimepigiwa kura na ukaguzi wa huduma duniani, ambapo Mtandao wa World Travel Awards 2023 umetoa tuzo za Ushindi kwa mchanganuo ufuatao;-

 

Miongoni mwa tunzo waliopita ni pamoja na kushindanishwa kwa Bodi za Utalii Barani Afrika (Africa’s leading Tourist Board) kwamba Bodi za nchi 12 za Botswana, Misri, Gambia, Ghana, Kenya, Morocco, Namibia, Nigeria, Rwanda, Afrika Kusini, na Zambia zilishindanishwa na iliyoibuka mshindi wa kwanza ni Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

 

Pili kakundi jingine ni la tenti za starehe zenye hadhi ya juu (Africa’s leading Luxury tented Safari camp) iliyoshinda barani Afrika ni Siringit-Serengeti Camp Tanzania.

 

Tatu,katika kundi la visiwa vipya venye hadhi ya juu kwa kuvutia watalii barani Afrika (Africa’s new leading Luxury Islands) ni kisiwa cha Thanda kilichoko katika wilaya ya Mafia Tanzania ndicho kimeongoza.

 

Nne, kundi la Hifadhi za Taifa Afrika (Africa’s Leading National Park) Hifadhi ya Serengeti imeongoza.

 

Tano, Sehemu za mapumziko (Africa’s Leading new Resorts) kwenye kundi hili mshindi barani Afrika ni Emerald Zanzibar Resort & Spa.

 

Sita, Kampuni inayoongoza Watalii (Africa’s leading Tour Operators) hapa makampuni mbalimbali 13 yalishindanishwa barani Afrika na iliyoibuka mshindi ni ZARA Tours ya Tanzania.

 

Saba, katika kundi la Eneo la uhifadhi lenye kuvutia Zaidi katika Afrika (Africa’s Leading Tourist attraction) hapa kwenye kundi hili eneo la Ngorongoro (NCA) limeibuka Mshindi.

 

Nane, pia kampuni mbalimbali ziliingia kwenye ushindi wa aina mbali mbali ndani ya nchi na zilizoongoza ni kampuni ya ndege ya Auric, na nyingine ni kama vile, “First Rental Tanzania”, Zanzibar Serena Hotel, Gran Melia Arusha, Melia Zanzibar, Twiga Tours, Lamai Serengeti, Kuro Tarangire. Makampuni mengine ni Green Inspirations DMC, Zara Tours, Satguru Travel Tanzania, FCM travel-Tanzania Skylink Travel & Tours na mengineyo.

 

Dkt. Mlay ameeleza kuwa ushindi huo unaendelea kuiweka Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.  Samia Suluhu Hassan kwenye ramani ya Dunia na kuongeza idadi kubwa ya watalii.

 

Hata hivyo, amesema TTB, inawashukuru sana, World Travel Awards na wadau wote walioshiriki katika mchakato mzima aliosababisha ushindi huo bila kuwasahau waliopiga kura na kuwezesha vivutio.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI