![]() |
| Mhe. Jerry Silaa; Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi |
Na Hamida Ramadhani Matukio Daima APP Dodoma
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa ameilekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kufanya uchunguzi dhidi watumishi 11 aliowasimamisha kazi ambao waliokuwa wakifanya kazi katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Dodoma baada ya kukutwa na tuhuma mbalimbali .
Pia ameita Taasisi hiyo kuchukua hatua stahiki kwa watimishi watakaobainika kwenye tuhuma hizo.
Maelekezo hayo ameyatoa Leo jijini hapa, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa maelekezo ya serikali kuhusu uboreshaji huduma za sekta ya ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Mwanza.
Amesema ktoba tatu mwaka huu serikali ilitoa maelekezo yaliyolenga kuboresha sekta ya ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Mwanza ambapo wizara imeanza kuchukua hatua ambapo imewasimamisha kazi watumishi wawili waliokuwa wakifanya kazi Mwanza na watumishi Tisa wa Jiji la Dodoma kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.
"TAKUKURU imefahamishwa kuendelea kuwachunguza watumishi hao na kuchukua hatua," Amesema Waziri huyo
Na kuongeza "Wizara inaendelea na uboreshaji wa Mifumo ya Kielekroniki wa Kutunza Taarifa za Ardhi (ILMIS) ili kuboresha utoaji wa huduma ikiwemo kurahisisha upatokanaji wa hati milki na utoaji wa huduma kwa wananchi kwa njia ya mtandao," Amesema
Amesema kuwa maboresho ya mfumo huo yanatarajiwa kukamilika mwaka huu mwishoni na kusambazwa nchi nzima.
"Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kushirikiana na ofisi ya ardhi waliendesha kliniki maalumu ambapo jumla ya wananchi 3,056 walihudumiwa. Hati milki 1,474 zilitolewa papo hapo na utaratibu huu umekuwa ukitekelezwa nchi nzima.
MAELEKEZO
Waziri Silaa ameilekeza Wizara kuzingatia waraka wa Wizara katika ulipaji wa fidia ambapo unasisitiza kutenga fedha kwa ajili ya kulipa fidia kabla ya Mthamini Mkuu kujiridhisha na majedwali ya kulipa fidia
Pia amesitisha utaratibu wa upimaji shirikishi katika Jiji la Dodoma na kutoa onyo kwa kamati ya mipango miji na mazingira ya Jiji la Dodoma na kuyasimamia mabalaza ya kata ili yawe na tija katika kushughulikia migogoro ya ardhi nchini.
"Wizara inaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na serikali kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali. Hatua hiyo itawezesha kuboresha utendaji kazi katika sekta ya Ardhi sio katika halmashauri ya Jiji la Dodoma na Mwanza bali katika halmashauri zote nchini,"alisema
mwisho






0 Comments