Header Ads Widget

POLISI MBEYA YANASA WAWILI KWA KUTUMIA JINA LA MO DEWJI KUTAPELI

 


Na Matukio Daima Media, Mbeya 

WATU wawili wakazi wa Chapakazi katika Mji mdogo wa Mbalizi Wilaya ya Mbeya Mjini wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kughushi Nyaraka kwa kutapeli watu kwa kutumia jina la "Mo Dewji foundation.



Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya,Benjamin Kuzaga amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa Octoba 22 mwaka huu  katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Altas  iliyopo katika Mji Mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya mjini katika misako inayooendelea katika maeneo mbalimbali.



Aidha Kamanda Kuzaga amewataja watuhumiwa hao kuwa ni ,Sarael Geshon (19) na Christiani  Erasto (21) ambao wote ni wakazi wa Chapakazi ambao walikamatwa katika nyumba ya kulala wageni ya Altas kwa tuhuma za  tuhuma za kughushi nyaraka mbalimbali na kutapeli watu kwa kutumia jina la “Mo Dewji foundation”.


Aidha Kamanda Kuzaga amesema watuhumiwa hao pia walikutwa  wakiwa na simu za mkononi smart phone 6, simu ndogo 3, line za simu za mtandao wa Vodacom 10, Tigo 2 na Airtel 3 zenye usajili wa majina tofauti wakizitumia kuibia watu mbalimbali kwa kutoa machapisho ya uongo kwamba wanatoa mikopo kupitia “Mo dewjifoundation”.


Watuhumiwa wamekuwa wakighushi kwa njia ya kompyuta kitambulisho cha NIDA, Tin ya TRA, leseni ya biashara na usajili wa Brela kwa jina la "Mo dewji foundation na kisha kutapeli watu wakidai kutoa mikopo kwa riba nafuu.


 Watuhumiwa wamekiri kutekeleza matukio ya utapeli katika maeneo mbalimbali na kujipatia kipato isivyo halali.


Mmoja wa wakazi wa Uyole Jijini Mbeya, Baraka  Atupele amesema watu kama hao wamekuwa wengi kwenye jamii ambao wamekuwa wakitumia majina ya watu wakubwa kutapeli watu na kujipatia fedha kwa njia isiyo halali .


"Nalipongeza jeshi la polisi kwa jitihada hizi,ombi letu sisi wananchi polisi iongoze nguvu ya msako kwani watu wa hivyo kwenye jamii wapo wengi ambao wamekutwa wakitumia kivuli cha viongozi wakubwa kutoka taasisi mbalimbali"amesema Mkazi huyo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI