Header Ads Widget

SIKU YA MAKAZI DUNIANI WADAU WA ARDHI WAADHIMISHA KWA MDAHALO WA KITAALUM

 


NA HAMIDA RAMADHAN , MATUKIO DAIMA APP DODOMA



WAZIRI wa Ardhi nyumbani na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa Amesema changamoto ya migogoro ya Ardhi kumesabaisha baadhi ya shughuli za uchumi kukwama kutokana na mipango miji mibovu


Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya makazi duniani leo October 2,2023 Jijini hapa,  Waziri huyo amesema Serikali inatumia siku hiyo kutafakari namna bora ya kuboresha hali ya makazi Katika miji na kuondokana na migogoro iliyopo.


Amesema Kwa kulitambua hilo Serikali ipo katika maboresho ya sera ya ardhi ambayo italeta suluhisho kwenye suala  la umiliki wa ardhi ikiwa ni pamoja na kuwashughulikia wamiliki wasioendeleza ardhi.


Amesema Maadhimisho hayo ni fursa Kwa wananchi na wadau wengine wa makazi kutafakari Kwa kila mmoja namna atakavyoshiriki kuboresha hali ya makazi na kutafakari kuhusu namna miji inavyoweza kukabiliana zinazoathiri uchumi.


" Lengo la Wizara ni kutoa huduma ya ugawaji viwanja viinavyoendana na huduma za jamii na kwamba matarajio hayo yatafufua uchumi wa pamoja," Amesema Waziri huyo.


Ameeleza Serikali itahakikisha inakuwa na mipango endelevu kwenye Sekta hiyo ili kukuza uchumi wa miji yenye tija na jumuishi ikiwa ni pamoja na kuwekeza miji endelevu ili kukuza nishati safi kulinda mifumo ikolojia.


"Tutaondokana na changamoto kwenye Sekta ya ardhi Kwa kuwezesha usanifu wa miji endelevu na mifumo mizuri ya utawala na makazi yenye mpangilio mzuri wa utawala wa ngazi mbalimbali ili kukuza biashara na utoaji huduma Kwa jamii,"amesema


Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  Anthony Sanga amesema Wizara inajipanga kufanikiwa kuondoa kero ya uvamizi holela na kwamba kama vizara tayari wamefanya tathmini kuainisha maeneo ya kutilia mkazo zaidi ikiwemo upimaji bora wa ardhi .



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI