Header Ads Widget

KAMPUNI YA SCANIA YAUNGA MKONO MAPAMBANO DHIDI YA MABADILIKO TABIANCHI

 


Kampuni ya kutengeneza magari ya Scania ya nchini Sweden imeadhimisha miaka 60 ya uwepo wake hapa nchini kwa kutambulisha gari linalotumia teknolojia ya gesi ikiwa ni juhudi za kampuni hiyo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuhamasisha matumizi ya nishati safi.


Utambulisho wa gari hilo umefanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo hapa nchini yaliyopo Vingunguti, Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.


Akiongea na wafanyakazi wa kampuni ya Scania Balozi wa Sweden nchini Charlotta Ozaki Macias ameeleza kuwa sanjari na uwepo wa kampuni hiyo pia Tanzania na Sweden zinaadhimisha miaka 60 ya ushirikiano baina ya nchi hizo huku kukiwa na mambo mengi ya kujivunia.



Balozi Macias alibainisha kuwa, kwa sasa Tanzania na Sweden zina changamoto tofauti ukilinganisha na zile zilizokuwepo miaka 60 iliyopita ingawa zote zinakabiliwa na tatizo la mabadiliko ya Tabianchi ambalo kwa sasa ni tatizo la kidunia.


Alieleza kuwa, hatua ya kampuni ya Scania kutengeneza magari yanayotumia gesi itatupunguza uharibifu wa mazingira na gharama za uendeshaji. Gari hilo lina uwezo wa kutembea kilometa 700 hadi 800 iwapo mitungi yake nane itajazwa gesi.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI