Header Ads Widget

RTO NDOZERO ATOA POLE KWA FAMILIA KWA MAJERUHI WA AJALI IRINGA

 

Mkuu wa kikosi Cha usalama barabarani mkoa wa Iringa Mosi Ndozero akimtembelea mmoja wa majeruhi wa Ajali 

RTO  Ndozero akitoa elimu ya usalama barabarani Kwa wananfunzi shule ya msingi Ruaha Mbuyuni A na B


Mkuu wa kikosi Cha usalama barabarani (RTO) mkoa wa Iringa Mosi Ndozero amefika kituo Afya Ruaha Mbuyuni wilaya ya Kilolo kumjulia hali Mwanafunzi majeruhi wa Ajali .

Watoto hao wa shule ya msingi Ruaha Mbuyuni wakiwa njiani kwenda shule waligongwa majira ya Saa 12:30 asubuhi Gari ndogo IT 9002 aina Mazda Demio lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda Tunduna.

Mkuu huyo wa usalama barabarani amefika kumjulia hali mwanafunzi huyo kutokana na Ajali ya gari iliyowafuata wanafunzi hao nje ya barabara na kuwagonga na kusababisha vifo vya watoto Wawili huku mmoja akijeruhiwa .

Ajali hiyo ilitokea eneo la Kware Ruaha Mbuyuni barabara kuu ya Morogoro -Iringa.

Pamoja na kutoa pole Kwa familia zilizopatwa na msiba huo pia akiwa kituo Cha Afya Ruaha Mbuyuni ametoa pole Kwa majeruhi wa Ajali hiyo .

Wakati huo huo RTO Ndozero amefanya ziara Katika shule ya msingi Ruaha Mbuyuni A na B Kitongoji Cha Kware kutoa elimu ya usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuwafundisha juu ya alama za usalama barabarani yakiwemo maeneo rasmi ya kuvuka Wenda Kwa miguu .


Hata hivyo alitoa onyo Kwa Madereva kuzingatia Sheria za usalama barabarani na kuepuka kuendesha Magari Kwa mwendo Mkali kwenye makazi ya watu .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI