Header Ads Widget

MNADA WA KWANZA WA KOROSHO WAFANYIKA TANDAHIMBA

 


Chama Kikuu cha Ushirika Tandahimba na Newala(TANECU) kimefanya Mnada wa kwanza wa zao la Korosho  kwa Msimu wa kilimo Cha Korosho 2023/2024  katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ambapo Korosho imeuzwa kwa Bei ya juu ya Tsh.2050 na Bei ya Chini Tsh.1950 Kwa kilo moja.


Mwenyekiti wa TANECU Karim Chipola amewasisitiza Wakulima kuziandaa Korosho kwa Ubora kabla ya kuzipeleka ghalani.


"Ukipeleka Korosho Mbichi ghalani inaharibu soko na kushusha Bei, niwasisitize endeleeni kuzikausha na kuepuka kuongeza vitu ambavyo siyo Korosho " Chipola



Akisoma hali ya Ukusanyaji wa Korosho kwa Mnada wa kwanza Meneja wa TANECU Mohamed Nassoro amesema Jumla ya Tani 7752  zimekusanywa ambapo kati ya hizo Tandahimba imekusanya Jumla ya Tani 5981.


Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba,Kaimu Katibu Tawala Wilaya  hiyo Francis Mkuti ameishukuru Serikali kwa kutoa Pembejeo kwa wakulima Bure hali iliyopelekea Uzalishaji wa Korosho kuongezeka.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI