Na Mwandishi wetu, Mtwara
Mabalozi wa usalama barabarani (RSA) wamezindua wiki ya mabalozi wa usalama barabarani kwakutoa elimu mashuleni na kwa baadhi ya watumiaji wa barabara wakiwemo watoto na madereva wa magari.
Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyofanyikia katika kiwanda cha saruji Dangote Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi RSA Mohamedi Mpinga alisema kuwa jitihada za kupambana dhidi ya ajali barabarani zinahitajika kwa kila mmoja kwani sasa zimeendelea kuleta athari kubwa ya vifo vya watu na uharibufu wa mali hasa barani Afrika.
Alisema kuwa kwa mujibu wa shirika la afya Duniani (WHO) asilimia 20 ya ajali zote barabarani ulimwenguni hutokea barani Afrika, mfano nchini Tanzania kwa mwaka 2022 pekee kulikuwa kuna ajali 1720 hizi ajali zilisababisha vifo 1545 na majaruhi 2278 hali ambayo inaongeza hatari kwa jamii yetu.
“Usalama barabarani ni tukio ambalo lina mgusa kila mtu kutokana na asili yake binadamu anasifa ya kujongea ambapo hufanya safari ya kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ambapo maendeleo ya sayansi uchumi na teknologia yamefanya binadamu kutafuta njia ya rahisi ya kutoka na kutafuta ambapo inahusisha vyombo vya moto na visivyo vya moto”
“Unajua safari zote hizi zinapita barabarani hakusiku binadamu atapata safari bila kutumia barabara iwe anakwenda ama anatoke sehemu yoyote anahitaji kuwa salama hapo ndio tunazungumzia dhana ya usalama barabarani kuwa ni jukumu letu sote” alisema Mpinga
Nae Mwenyekiti wa mabalozi wa usalama barabarani mkoa wa Mtwara Nassoro Mansour alisema kuwa baada ya kufanya shughuli mbalimbali za uelimishaji na zinginezo zinazohusu masuala ya usalama barabarani huandaliwa siku maalum kwa ajili ya wadau kukutana pamoja kujadiliana masuala mbalimbali yanahusu usalama barabarani ambayo itafanyikia mkoni hapa.
Mwakilishi wa Kamanda Polisi wa usalama barabarani mkoa wa Mtwara Almasi Juakali amesema kuwa unapokuwa katika matumizi ya barabara kila mmoja atimize wajibu wake.
"Ukiwa safarini unabadilika jina kulingana na safari unaweza kuitwa mwenda kwa miguu, abiria na dereva kitu kikubwa ukiwa barabarani unatakiwa kujali wengine ambao hawautmii chombo kama chako"
"Tuweke shida pembeni ili kuweza kudhibiti ajali za barabarani madereva jiepusheni na ajali nyingi ambazo zinasababishwa na mambo mbalimbali ukiona unatatizo pumzika kwa muda ili utumie kwa usalama zaidi tuwashauri madereva kuhusu chombo ili kupunguza ajali zisizo na ulazima hasa mwendo kasi ama ubovu wa gari" alisema Juakali
0 Comments