Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack ameagiza viongozi wa kilimo na vyama vya ushirika kusimamia ukusanyaji wa korosho iliyo safi na bora Kwa ajili ya kwenda sokoni
Akizungumza wakati wa kikao kazi cha viongozi mbalimbali wa kilimo mkoa wa Lindi alisema kuwa hawatapokea wala kupeleka mnadani kutokana na uchafu huo ambao unaharibu soko la korosho mkoa wa Lindi.
Telack ameagiza kuwepo na usimamizi mzuri wa kupata korosho zilizo bora sokoni na kuitangaza korosho ya mkoa wa Lindi kuwa ndio korosho Bora sokoni.
0 Comments