Header Ads Widget

RAIS SAMIA AHITIMISHA ZIARA YAKE YA SIKU TATU MKOANI SINGIDA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba ya mwisho wakati akihitimisha ziara yake ya siku tatu mkoani Singida


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameendelea na ziara yake mkoani Singida siku ya leo oktoba 17 ambapo amehitimisha katika wilaya ya Iramba.


Katika ziara yake siku ya mwisho mkoani hapo Mheshimiwa Rais Samia amepokea taarifa ya Mradi wa Umeme Vijijini REA awamu ya tatu mzunguko wa pili pia amezungumza na wananchi wa Wilaya ya Iramba, katika eneo la Shule ya Msingi Shelui.


Akitoa salamu za shukrani kwa Rais, Mkuu wa mkoa wa Singida Mheshimiwa, Peter Joseph Serukamba anasema "Mheshimiwa Rais, sisi watu wa Singida tuna deni kwako na tunaomba utukubalie deni hili tutalilipa kwa awamu mbili, ya kwanza tutalipa mwaka kesho 2024 na awamu ya pili kwa kuwa tutakuwa tumechelewa kulipa tutalipa mwaka 2025. Wananchi wa Singida watakuchagua wewe kuwa Rais kwa kura nyigi sana" 


Katika hotuba yake Rais Samia ameeleza kuwa ziara yake ndani ya mkoa wa Singida imekuwa na mafaniko makubwa kwani mbali na kuelewa changamoto zinazowakabili wana Singida, katika ziara hii amekagua kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya elimu.  Alizindua shule ya msingi mpya ya kisasa kabisa Imbele manispaa ya Singida.


Lakini pia amefanyia kazi miradi  ya barabara na miundo mbinu na katika suala la miradi ya miundo mbinu amezindua mradi wa daraja la Msingi utakao  kwenda kuunganisha mkoa wa Singida na mikoa mingine ya Simiyu, Tabora na mikoa mingine iliyo jirani na mkoa wa Singida.


Aidha Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefurahishwa na jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali katika kutekeleza Kampeni ya "kumtua mama ndoo kichwani" ambapo wananchi kwa asilimia kubwa wanafaidika na kazi inayofanywa na serikali kupitia Wizara ya maji katika  kuboresha upatikanaji wa maji nchini.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI