Header Ads Widget

MUFTI NA SHEIKH MKUU WA TANZANIAWAKITANA NA VIONGOZI WA CHUO CHA HIJAZ

 



Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Alhaj Dkt. Aboubakar Zubeiry bin Ally na ujumbe wake wa BAKWATA pamoja na viongozi wa Jumuiya za Waislamu waishio Uingereza wakiwa na viongozi wa Chuo cha Hijaz kilichopo Nuneaton. 


Chuo hicho kinachoongozwa Sheikh Faizul Saddick ni kituo kikubwa cha kiroho katika ulimwengu wa Magharibi, kinachotoa fursa kwa watu wote  kujionea ukarimu wa Kiislamu na kujifunza kuhusu Uislamu.


Nuneaton ni mji wa soko katika eneo la Nuneaton na Bedworth kaskazini mwa Warwickhire, Uingereza, iliyoko karibu na mpaka wa kaunti na Leicestershire kaskazini-mashariki.


Mufti na Sheikh Mkuu na ujumbe wake, walio katika hatua ya mwishoni wa ziara yao nchini Uingereza, wamefika Hijaz College kujifunza mengi katika dini ya Kiislamu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI