Header Ads Widget

LEO KATIKA HISTORIA OCTOBER 14 KUMBUKIZI YA MWL NYERERE

 


Kutoka kwa Mwl wangu wa mambo ya kimbingu na historia ya Dunia 

Na Comred Mkakia Issa


Barua ya Mwl Nyerere aliyoiandika kwa Father Lynch pale St. Francis Pugu, kuomba kujiuzulu kazi ya ualimu ili akakijenge chama cha TANU, ili kupigania Uhuru wa Tanganyika kutoka kwa wakoloni.


Mkuu wa shule

St. Francis college

Pugu.


  Mpendwa baba Lynch


       Nimeamua kuzingatia chaguo ulilonieleza mimi, kati ya kazi yangu hapa shuleni na uanachama wangu wa TANU, na nimefikia maamuzi kwamba lazima nijiuzulu kwenye nafasi yangu hii ya shule.


Lakini sasa nimegundua nimewakilisha Kwako chaguo sawa na lililo sahihi, sababu shughuli za TANU zinaingiliana na kazi zangu za shule ingawa ni tatizo langu binafsi, na si muda mrefu au baadae nitapunguza shughuli zangu za kwenye TANU au kuchukua chaguo langu kati ya TANU na shule, kwenye jambo hilo uchaguzi wangu huu utakuwa ni wa kweli, na kama nitafahamu kwamba siwezi kufanya kazi zote hizi mbili kwa pamoja kikamilifu, basi nitaachana na kazi za shule na kuijenga TANU, Lakini sidhani kama kujiuzulu kwangu na kwenda TANU utanipa mimi masharti ya kuendelea na kazi. Nani hapa Tanganyika yupo huru au kidogo yupo huru kiasi kuliko walimu wa misheni, 


Lakini kama Uhuru wa walimu wa misheni ulikuwa unatiliwa mashaka, nafasi yao itakuwa ni giza. kwangu mimi siwezi kuona sababu yoyote kwanini kila mwajiri  asiwape watumishi wake masharti sawa, na kwamba uwezekano utakuwa ni matatizo, kujiuzulu ni lazima, kwahiyo najiuzulu kama njia ya kupinga suala hilo.


Samahani, ni kwamba shughuli zangu ndani ya TANU kiukweli  zinaharibu uwezo wangu wa kufundisha, samahani kuhusu usumbufu ambao kujiuzulu kwangu kwa lazima kwa kipindi kifupi utakusababishia wewe na marafiki zangu, nina simanzi kuhusu matokeo ya uchumi yajayo kwenye familia yangu.


Kama ningekuwa kwenye nafasi yako ,Baba Lynch, ningetenda njia Sawa ileile kama ulivyotenda, Tumaini langu pekee ni kwamba utafikiri inawezekana kwamba ungekuwa kwenye nafasi yangu ungelichukua maamuzi sawa kama nilivyochukua.

Nakushukuru wewe na baba wengine kwa wema mlionitendea, nitaomba maombi yenu zaidi kuliko nilivyofanya huko nyuma, endelea, Baba, kuniombea.


Kijana wako mpendwa kwa kristu.

                

                                                     Julius Nyerere.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS