![]() |
Stella Mwarwa; Meneja wa shirika la bima NIC Kanda ya Ziwa |
NA CHAUSIKU SAID, MATUKIO DAIMA APP MWANZA
Jamii imeshauriwa kukata bima za majanga mbalimbali ikiwemo ya vyombo vya moto itakayowasidia kupunguza madhara yanapotokea kwenye jamii.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa shirika la bima NIC Kanda ya Ziwa Stella Mwarwa na kueleza kuwa faida kubwa ya kukata bima ni kuondokana na wasiwasi kipindi ambacho mtu hupatwa na majanga yeyote yale.
Stella Amesema kuwa bima ya vyombo vya moto pamoja na nyumba inaweza kuwasidia wananchi kuwalinda kipindi wanapopatwa na majanga yasiyozuilika kama mafuriko, na nyumba kuungua moto
"Hivi karibuni tunategemea mvua kunyesha ukiwa na hiyo bima inakusaidia sana, lakini pia juzi tu hapo tulishuhudia Mkoani kwetu hapa ajali ilitokea wakati kikundi Cha mchakamchaka wakifanya mazoezi waligongwa na gari na kufariki bahati mbaya watu wale hawakuwa na bima ya kuweza kuwasidia pia hata mwenye gari nae hakuwa na bima ambayo ingeweza kumsaidia kutengeneza gari" Alisema Stella.
Aidha ameeleza kuwa Kila mwananchi anapaswa kukata bima na sio kusuburi apatwe na majanga ndipo aanze kulalamikia serikali nakuomba imsaidie baada ya kupata majanga.
"Ukiwa umekata bima ya nyumba inaweza kukusaidia kukihamisha kutoka sehemu ya mafuriko na kwenda sehemu nyingine.
0 Comments