Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imesema uhusiano wa Tanzania na Zimbabwe katika sekta za biashara na uchukuzi utaendelea kuwaimarishwa baada ya kufanyakazi kwa pamoja ili kupata ufumbuzi wa kero na changamoto zinazokwamisha kasi ya kukua kwa biashara katika ushoroba wa Dar es Salaam.
Maazimio hayo yalifikiwa Oktoba 16, 2023 kati ya Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Zimbabwe, Mhandisi Joy Makumbe kuthibitisha Nia ya serikali zao kuimarisha uhusiano wa kihistoria.
Aidha, wawakilishi hao wa Serikali hizo, walifikia maamuzi hayo wakati wa hafla ya ufunguzi wa ofisi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), mjini Harare, nchini Zimbabwe.
"Tanzania na Zimbabwe inatumia fursa za kiuchumi zilizopo katika pande zote mbili kwa manufaa ya wananchi wetu" alisema Profesa Mbarawa.
Mwisho
0 Comments