Header Ads Widget

ALIYEMUUWA MWANAE KWA KUMCHOMA MOTO NA MAFUTA YA TAA ATIWA MBARONI.

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limefanikiwa kumkamata mama mmoja aitwae Semeni Halfani (45) mkazi wa kitongoji cha Reli juu wilayani Mwanga kwa tuhuma za kumsababishia kifo mwanae wa kumzaa aitwae Shamsidin Msemo(13), kwa kumwagia mafuta ya taa huku akiwa amemfunga mikono na kumchoma moto.


Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa alisema kuwa, baada za juhudi za muda mrefu kwa kushirikiana na Wananchi wema walifanikiwa kumkamata mama huyo Ifakara mkoani Morogoro alipokuwa amekimbilia kwenda kujificha.


Kamanda Maigwa alisema kuwa mnamo Agosti 31 mwaka majira ya saa kumi na moja jioni nyumbani kwa mtuhumiwa alimtuhumu mtoto wake huyo kuchukua viazi vya kukaanga chipsi bila ruhusa ya mama yake pamoja na fedha shilingi elfu hishirini hali iliyopelea kumfunga kamba na kummwagia mafuta ya taa kasha kumchoma moto na kusababisha majeraha makubwa na kupelekea kifo chake wakati akiendelea na matibabu katika hospitali ya rufaa ya KCMC Oktoba 03 mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI