Header Ads Widget

WAWEKEZAJI WAZAWA WATAKIWA KUENDANA NA KASI YA RAIS DKT SAMIA

 


Na fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar


Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji amewataka wawekezaji wazawa ambao wamepewa zabuni ya kuchimba makaa ya mawe katika mradi wa Mchuchuma Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe kufanya kazi kwa weledi mkubwa ili kufikia malengo ya Serikali ya uendelezaji wa miradi ya Kimkakati.

 

Wito huo ameitoa Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya utiaji saini wa Mikataba ya makubaliano kati ya Makampuni matano ya Wazawa na Shirika la Taifa la Maendeleo( NDC) ambayo yatatekeleza mradi wa Liganga na Mchuchuma kwakua ni maendelezo ya maono ya Serikali ya awamu ya sita ya kuendeleza sekta ya Viwanda na Biashara  hapa nchini.


Amesema kuwa, kwamba kwa nyakati tofauti Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa akisema  ni wakati sasa umefika kwa rasilimali iliyopo katika miradi ya kimkakati ya Liganga na Mchuchuma kuanza uzalishaji na kwamba ni shauku yake kuona mradi huo wa muda mrefu unatekelezwa.


 Aidha amesema kwamba Rais Dkt Samia Suluhu Hassan tayari ameridhia kutoa kiasi cha shilingi bilioni 15.4 ikiwa ni malipo ya fidia kwa wananchi wapatao 1142 ambao watapisha utekelezaji wa mradi huo ambao unatarajiwa kuanza kwa kufanyika utafiti  mapema mwezi huu.



Kwa upande wake, Mkurugenzi Mwendeshaji wa shirika la Taifa la Maendeleo ( NDC) Dkt Nocolaus Shombe amesema kuwa awali mchakato huo ulihusisha jumla ya Kampuni ishirini na tano (25) ambapo jumla ya kampuni kumi na saba( 17) zilifanikiwa kuwasilisha maombi yao kwa ajili ya uchambuzi na ushindani na hatimaye zilipatikana kampuni tano zilizokidhi vigezo.

 

"Kampuni ishirini na tano zilipewa nyaraka za zabuni kupitia mfumo wa ununuzi serikalini ( TANePS) ambapo kampuni 17 zilifanikiwa kuwasilisha nyaraka za zabuni,nakwamba kila kampuni itazalisha tani 30 kila mwezi sawa na tani 150 kwa kampuni zote tano kwa mwezi "amesema Dkt Shombe.

 

Dkt Shombe ameendelea kusema kuwa mradi huo utakua na manufaa makubwa kiuchumi ikiwemo kutoa ajira zaidi ya mia tano za moja kwa moja, 500 ikirahisisha upatikanaji wa nishati inayotokana na makaa ya mawe kwa Viwanda hali ambayo itachochea ukuaji wa viwanda nchini pamoja na kuingiza fedha za kigeni kwa mkaa utakaouzwa nje ya nchi hususani nchi za jirani.

 

Jumla ya kampuni tano zimetia saini makubaliano hayo ya uchimbaji wa makaa ya mawe katika mradi wa Mchuchuma ambazo ni Sheby Mix Investment Limited ,Nipo Engineering Company Limited,Chusa Mining Company Limited ,Kindaini Company Limited na Cleveland Mine and Service Company Limited ,mkataba ambao utadumu kwa muda wa miaka mitano.



Akizungumza kwa niaba ya Mchimbaji na Mwekezaji wa Madini kutoka kampuni ya Cleveland Minging and Cervice Compan, Ndaisaba George Luhoro amesema kwa sasa wanaenda kuandika historia na kuongeza ajira katika pato la taifa kwa makaa ya mawe waliyokuwa wanayasikia toka wazaliwe sasa wanaenda kuyachimba.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI