Header Ads Widget

WATATU WAFARIKI KWENYE MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI NACHINGWEA.


Matukio Daima App, Nachingwea.

Wafugaji wawili na mkulima mmoja wamefariki kwenye mapigano yaliyotokea katika mpaka wa wilaya ya Nachingwea na Tunduru kutokana na ugomvi wa ardhi


Amethibitisha kutokea kwa vifo vya wafugaji wawili,Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo  alisema kuwa vifo hivyo vinatokana na kupigwa na watu wanaodaiwa kuwa ni wa jamii ya wakulima kutoka katika Kijiji cha Tinginya wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma waliovamia eneo la marisho la kijiji cha Matekwe lililotegwa Kwa ajili ya wafugaji.


Moyo alisema Wafugaji waliofariki ni Nyerere kisingweda 80,na kidabeleda Miaka 31 wote walikuwa wakiishi katika Kijiji cha Matekwe katika eneo lililotengwa Kwa ajili ya matumizi ya ufugaji.


Katika mkutano wa Adhara uliowaunganisha wakuu wa wilaya wa sehemu hizo mbili, Moyo amewataka wahusika wa tukio hilo kujisalimisha wenyewe Mikononi mwa jeshi la Polisi kwani kwa namna yoyote amesema ni lazima wapatikane na hatua za kisheria zifwate kwa wote walioshiriki kuwaua na kupanga njama za mauwaji kwa wafugaji


Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro alisema kuwa hawapota tayari kumvumilia mtu yeyote yule atakayesabisha uvunjifu wa amani katika wilaya ya Tunduru 


Mtatiro alisema kuwa mkulima aliyefariki alikuwa najulikana kwa jina la Fadhili Nakulamba  miaka 32 mkazi wa Kijiji cha Tinginya

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS