Header Ads Widget

WACHEZAJI WA MOROCCO WACHANGIA DAMU KWA WAHANGA WA TETEMEKO.


Na Simon Joshua - Matukio Daima App. Morocco.

Wachezaji wa mchezo wa Soka nchini Morocco wamejitokeza kuchangia damu ikiwa ni harakati za uokoaji wa majeruhi na wahanga wa tetemeko la ardhi lililoikumba nchi ya Morocco siku ya juzi.


"Kipaumbele ni kutoa damu kwa wale walio katika hali mbaya. Kuchangia damu ni jukumu la kila mtu kuokoa maisha ya watu wengi iwezekanavyo." Amesema Achraf Hakimi, Nahodha wa timu ya taifa ya Morocco.


Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani, hadi sasa Watu 2,012 wamefariki dunia huku wengine 2,059 wakijeruhiwa na 1,404 wako katika hali mbaya kiafya.


Shirika la Afya Duniani limesema zaidi ya Watu 300,000 wameathirika na Tetemeko hilo lililopiga maeneo kadhaa ya Jiji la Marrakech ikiwemo Kijiji cha Asni ambacho kielezwa kuharibiwa karibia nyumba zote


Ni Tetemeko la pili kusababisha maafa makubwa ndani ya mwaka mmoja ambapo Miezi 7 iliyopita, takriban watu 50,000 walipoteza maisha kwa kupigwa na Tetemeko Nchini Uturuki.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS