Header Ads Widget

SERIKALI YAAHIDI KUKAMILISHA BARABARA YA KIBOROLONI - TSUDUNI - KIDIA KWA KIWANGO CHA LAMI..



NA WILLIUM PAUL.

SERIKALI imeahidi kukamilisha ujenzi wa barabara ya Kiboroloni- Tsuduni- Kidia kwa kiwango cha lami katika kipande kilichobaki ambapo itachangia kuongeza pato la Taifa kutoka na kutumika na watalii kupanda mlima Kilimanjaro kupitia lango la Kidia.


Hatua hiyo imekuja baada ya Mbunge wa Jimbo la Moshi vijijini wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro , Prof  Patrick Ndakidemi kuhoji bungeni je Serikali inamkakati gani wa kukamilisha barabara ya Kiboroloni-Tsuduni-Kidia kwa kiwango cha lami kwa sababu itarahisisha kupeleka watalii wanaopanda mlima Kilimanjaro kupitia lango la Kidia.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya alisema kuwa, barabara hiyo kwa sasa inasimamiwa na Wakala wa barabara nchini Tanroad mkoa wa Kilimanjaro.

Alisema kuwa, barabara hiyo imekuwa ikipangiwa fedha za ujenzi kwa kiwango cha lami kwa awamu hivyo Wizara wataangalia ukubwa wake ili kama itawezekana kuongeza fedha ili kipande kilichobaki kiweze kukamilika kwa kiwango cha lami.

 Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI