Header Ads Widget

SERIKALI NJOMBE YAAHIDI KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA WANANCHI.

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Serikali wilayani Njombe imeahidi kuendelea kutatua changamoto za wananchi katika sekta zote kama ilani ya CCM inavyoeleza ili kufikia malengo ya kusogeza huduma karibu na wananchi.


Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Njombe Mhe.Kissa Kasongwa wakati akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kusomwa kwa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha mapinduzi katika wilaya hiyo.


Awali Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  CCM Wilaya ya Njombe Justine Nusulupila amewataka watumishi wa serikali kuwahudumia wananchi na kutatua kero mbambali zinazoikumba jamii.



Naye Mbunge wa jimbo la Njombe Mjini Mhe.Deo Mwanyika amesema ujenzi wa mradi wa barabara ya zege ya Iton-Lusitu inayoendelea kutekelezwa ni moja ya sababu ya mradi mkubwa wa maji wa Igongwi kuchelewa kukamilika.


Aidha Mhe. Mwanyika amesema mpaka sasa mradi huo umetekelezwa kwa asilimia 99 lakini kumekuwa na changamoto ya kukatwa mabomba na mkandarasi anayetekeleza mradi wa barabara jambo linalosababisha wananchi kuchelewa kupata maji.


Ameongeza kuwa changamoto ya wananchi wa kijiji cha Luvuyo wilaya ya Ludewa kuzuia mradi huo usipite katika kijiji hicho mpaka mradi wao wa maji ukamilike kwasasa sio changamoto tena.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI