Header Ads Widget

MBUNIFU ATENGENEZA KIWANDA CHA KUTENGENEZA PETROL KWA KUTUMIA ‘PLASTIC’


Na Simon Joshua - Matukio Daima App, Dodoma.

Ikiwa Sayansi na teknolojia ikiendelea kukua duniani kote, ndivyo maisha ya mwanadamu yanavyozidi kuwa rahisi siku hadi siku.


Sayansi na teknolojia ndiyo iliyomfanya Kijana Samson Jumanne, Mbunifu aliyepata wazo la kutengeneza mafuta ya Petrol Kwa kutumia Ndoo za plastic na Matairi. Huyu ni Msomi wa  Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambaye hakuweza kufika mbali kutokana na kukosa sapoti ya ada kumaliza masomo yake chuoni hapo na kuamua kuacha Chuo.


Hii ni Teknolojia ambayo kama Serikali na wadau wataitilia maanani, basi inaweza ikapunguza kwa kiasi kikubwa kasi ya uharibifu wa mazingira duniani kwa kuchimba mafuta na kutengeneza mafuta kwa kutumia plastiki mbovu mtaani. 

Samson anasema mwanzo alikabiliwa na shutuma kutoka kwa wananchi ambao wanamzunguka waliodhania anapika pombe ya kienyeji maarufu kwa jina la ‘gongo’.


"Kwa Dodoma naishi Mtaa wa Mbwanga, Miyuji nilipokuwa anatengeza mtambo wangu watu walisema natengeza Gongo nilifunga na kuacha kutengeneza baada Mwenyekiti wa Mtaa kuniitia na kuniuliza ninachotengeneza, nilimweleza alinielewa nikaendelea kufanya uzalishaji" Samson Jumanne, Mbunifu wa wa kiwanda cha mafuta ya Petrol.


Umaskini umekuwa chanzo kikubwa kwa jamii ya Watanzania kwani hukatisha ndoto za vijana wengi wabunifu na wenye maono makubwa hasa katika nchi za ukanda wa jangwa la Sahara.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS