Header Ads Widget

WAKADIRIAJI MAJENZI WAOMBA KUTHAMINIWA ILI MIRADI KUKAMILIKA KWA WAKATI 


Na Thabit Madai - Matukio Daima App, Zanzibar.

TAASISI za Serikali na Binafsi zimeshauriwa kuwatumia Wakadiriaji Majenzi kabla ya kuanza utekelezaji wa Miradi ya mbalimbali ili kukamilisha kwa wakati miradi pamoja na kuokoa gharama zisizo za lazima.


Mkurugenzi wa Ujenzi wa Viwanja vya Ndege Injinia Mwanahamisi Kitego alipokuwa akisoma hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Tanzania Balozi, Mhandisi Aisha Amour wakati akifungua Mkutano wa 29 wa  Taasisi ya Wakadiriaji Majenzi Nchini ambao unaenda sambamba na Uchaguzi wa Viongozi wa Taasisi hiyo.


Alisema ni vyema kwa Taasisi kuwatumia Wakadiriaji ili kuondoa changamoto ya kukamilika kwa Miradi pamoja na gharama za uendeshaji wa Miradi.


Aidha alisema, mkadiria majengo ni mtu muhimu katika ujenzi kwani mtu wa kwanza kuulizwa yeye pamoja na mkataba juu ya utekelezaji wake.


Hivyo, aliwataka Wakadiriaji Majengo kufanya kazi kwa kuzingatia Maadili ya kazi hiyo kwa lengo la kuokoa fedha katika miradi mbalimbali ya Serikali na Binafsi.


Sambamba na hayo, alisema serikali itaendelea kufanya nao kazi na kuwasisitiza kuendelea kuwa waadilifu ili kutumia fedha zilizopangwa katika miradi sambamba na kuepusha hasara juu ya miradi inayoendelea kufanyika.

"Serikali zote mbili imejikita zaidi kuona mafanikio yanafikiwa kutokana na uchumi kupitia maeneo mbalimbali ikiwemo ujenzi na miundombinu mbalimbali na sekta binafsi" alisema.


Mapema, Rais wa Taasisi ya Wakadiriaji Majenzi Tanzania TIQS, Benard Ndakidemi ameiomba Serikali kutoa nafasi za Ajira kwa Wakadiriaji Majenzi katika Taasisi za Serikali ili kutoa Ushauri wa Mikataba ya Ujenzi wa Miradi na kuongeza Ufanisi.


Alisema, kumekuwepo kwa taarifa ya kuwepo sitofahamu katika ujenzi hivyo, alisema taasisi yao ipo tayari kutoa msaada wowote endapo serikali itahitaji.


Sambamba na hayo, aliziomba taasisi za serikali kuhakikisha miradi yao inatekelezwa kuhakikisha uwepo wa wakadiriaji majengo ili kuweza kupata thamani halisi ya fedha zitakazotumika.


Nao washiriki wa Mkutano huo wameeleza changamoto mbalimbali zinazowakabili wakadiriaji Majengo Nchini, ikiwemo, kutojulikana fani yao jambo ambalo litakapofanyika jambo serikali inakuwa haijui nani wa kumfata hasa katika kusimamia mikataba ya ujenzi.


Afisa uhusiano wa taasisi ya TIQS Geofrey Nyaluke, alisema, wao mara nyingi huwa wanasimamia kiwango na ubora wa mradi, mradi unakamilika kwa harama inayotakiwa na mtu anayeweza kuona ni mradi unakuwa bora zaidi ni mkadiriaji majengo.


Hivyo, aliomba serikali kuwapa kazi kwani wanaweza kufanya kazi kwa bidii na kuweka makadirio yaliyokuwa bora zaidi.


Nae, mkadiriaji majenzi kutoka Wizara ya Afya, QS, Amina Habibu, alisema, katika mkutano huo matarajio yao ni kuendelea kupata elimu zaidi na kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi.


Alisema, mara nyingi wanakuwa wanajenga bila ya kuwepo mkadiriaji majengo kwani ataweza kuwashauri juu ya mradi wao na kupunguza harama iliyokuwa bora.


Mkutano huo umehudhuriwa na Wajumbe wa Taasisi hiyo zaidi ya 400 Kutoka Mikoa yote ya Tanzania pamoja na Waalikwa kutoka Mataifa zaidi ya matano.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI