Header Ads Widget

IDADI YA VIFO VYA TETEMEKO VYAFIKIA 2000 MOROCCO.


Na Simon Joshua - Matukio Daima App, Morocco.

Idadi ya waliofariki kwenye tetemeko la ardhi nchini Morocco imeongezeka hadi kufikia watu zaidi ya 2,000.


Wizara ya mambo ya ndani inasema zaidi ya 1,400 wamejeruhiwa vibaya, na majeruhi wengi zaidi wako katika majimbo ya kusini mwa Marrakesh.


Mfalme Mohammed VI alitangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa na kuamuru kupelekwa makazi, chakula na msaada mwingine kwa walionusurika.


Tetemeko hilo la kipimo cha 6.8 lilipiga Marrakesh na miji mingi Ijumaa usiku. Katika maeneo ya mbali ya milima, vijiji vizima vinaripotiwa kusambaratika.


Kutoka kaatika Milima ya Juu ya Atlas, 71km (maili 44) kusini-magharibi mwa Marrakesh - jiji lenye hadhi ya urithi wa dunia ambayo ni maarufu kwa watalii.


Lakini mitetemeko hiyo pia ilisikika katika mji mkuu wa Rabat, ulio umbali wa kilomita 350, pamoja na Casablanca, Agadir na Essaouira.


Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak amesema Uingereza ilikuwa tayari kuisaida Morocco. "Tunaungana na kila mmoja aliyeathiriwa na tetemeko mbaya la ardhi huko Morocco jana usiku.

"Uingereza iko tayari kusaidia marafiki zetu wa Morocco," alisema katika ujumbe kwenye mtandao wa X, zamani ikijulikana kama Twitter.


Wakati huo huo Shirika la misaada la Uingereza liko tayari kutuma timu ya waokoaji nchini Morocco.


Mark Scorer, mkurugenzi wa operesheni katika Saraid, aliiambia BBC kuwa wako tayari kusaidia ikiwa itahitajika - kama walivyofanya mapema mwaka huu kufuatia tetemeko la ardhi lililokumba Uturuki.


Scorer alisema waokoaji wanaweza kuanza kutoa ushauri na usaidizi wa kitaalamu ndani ya saa 12 hadi 24.


Morocco iliwahi kushuhudia matetemeko makubwa ya ardhi hapo awali, ikiwa ni pamoja na mwaka wa 2004.


Tetemeko la ardhi lilipiga al-Hoceima kaskazini-mashariki mwa Morocco na kuua watu 628. Na mnamo 1960, tetemeko la ardhi la Agadir liliua watu 12,000.


Hilo linaweza kutoa kielelezo kidogo cha ukubwa wa majeruhi ambao tunaweza kuona katika tetemeko hili la ardhi.


Kitovu cha tetemeko la ardhi jana usiku kilikuwa katika Milima ya Atlas. Kuna vijiji vingi vya mbali ambavyo ni vigumu kufikia.


Inaweza kuchukua siku nyingi kabla ya sisi kujua hasa ukubwa wa janga hili kubwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS