Na Mbaruku Yusuph - Matukio Daima App, Tanga.
WANAWAKE wametakiwa kufanya jitihada za kuingia kwenye mfumo rasmi wa urasimishaji wa biashara zao ili waweze kuingia katika ushindani na kukubalika.
Hayo yamedhihirishwa na Mh:Mhandisi Aisha Ulenge alipofanya mahojiano maalum na vyombo vya habari juu ya dhamira ya kufanya Kongamano la wanawake na manunuzi ya Umma linalofanyika Jijini Tanga.
Mhandisi Ulenge alisema lengo la kongamano hilo ni kumsaidia mwanamke aweze kuingia kwenye fursa zilizo rasmi zinazowahitaji wao katika mfumo wa manunuzi ya umma kwa upana wake na fursa za biashara kwenye Bombala mafuta.
Alisema kongamano hilo pia limedhamiria kuwatoa wanawake wafanyabiashara kwenye mfumo wao wa zamani wa local na kuwabadilisha ili wawe katika mfumo wa Kampuni zitakazokuwa na majina rasmi ambazo zitasajiliwa na Brella ili waweze kuingia kwenye ushindani.
Alisema asilimia kubwa ya wanawake wamekuwa wakifanya biashara katika vikundi vyao ambapo wanakosa fursa za kujiendeleza kutokana na biashara zao sio rasmi na kuwafanya washindwe kukuza biashara zao na pato lao kwa ujumla.
"Tupo hapa na tunataka tuwafundishe wanawake wa Mkoa mzima wa Tanga na tunashirikiana na mashirika yote ya usajili ambayo tutakuwa nayo hapa kwa siku mbili kwa ajili ya wananawake hao waweze kurasimisha biashara zao"Alisema Mhandisi Ulenge.
Aidha alisema asilimia 80 ya bajeti ya Tanzania kila mwaka inakwenda kwenye manunuzi ya Umma hivyo inaleta maana ya uwepo wa fursa kwa wanawake ikiwa wataelimishwa ili waweze kuchangamkia fursa hiyo ya manunuzi kwa uchumi endelevu wa Taifa.
Alisema kongamano hilo limepewa jina la daraja conference litakalo wavusha wanawake toka walipo na kwenda mbele zaidi kimaendeleo na kufanya hivyo ni kuunga mkono jitihada za kuunga mkono matamanio ya Mh, Rais Samia ya kutamani wanawake kukua kiuchumi.
"Mimi kama mbunge mwanamke niliyepewa dhamana na wanawake wa Tanzania kupitia wanawake wa Mkoa wa Tanga nimeona nibebe maono haya na kufanya jitihada za kumfanya mwanamke anaingia kwenye mfumo rasmi wa kibiashara ili watu wote wanufaike na keki ya Taifa"Alisema.
Alisema fursa ambazo zipo katika mradi wa bomba la mafuta ni pamoja na mbogamboga,vyakula na swala la ushonaji wa sare za makampuni yanayofanya kazi katika mradi huo.
Hata hivyi amisema Kongamano hilo linafanyika Mkoani hapa kwa siku mbili ambapo limehudhuriwa na wanawake toka Wilaya zote za Mkoa ambapo Mgeni Rasmi anatakuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambae pia anazindua Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Ng'arisha Maisha itakayowahudumia wanawake wa Tanga na Tanzania kwa ujumla.








0 Comments