Header Ads Widget

WANANCHI WAMSHUKURU RAIS SAMIA

 



NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR 


WANANCHI na wafanyabishara mbalimbali wamemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwani amewapa fursa mbalimbali ikiwemo kutangaza biashara zao kupitia tamasha la kizimkazi.



Wakizungumza katika tamasha hilo, wananchi hao wamesema, wamekuwa na faraja na kuona kiongozi wao amekuwa akiwathamini na kuonesha utu aliokuwa nao kwa wananchi wote na wa mkoa wa kusini kwa ujumla.



Mmoja wa wananchi hao, Mwashamba Khatib Pandu, mkaazi wa Kizimkazi,  alisema wataendelea kumuunga mkono katika kutangaza mazuri yote anayoyafanya kwani amekuwa akitatua changamoto za wananchi kwa wakati bila ya ubaguzi na kuendelea kuwajali.



Alisema tokea kuja tamasha wamepata faraja kwa wananchi wa kizimkazi kwa mwaka jana wamepata ngalawa, na biashara zao zimekuwa zinakwenda vizuri huku akisisitiza kuwa uchumi umeengezeka kwani wageni mbalimbali wamekuwa wakipita katika kijiji chao.



Alisema, tokea kuanzishwa kwa tamasha wamekuwa wakinufaika na masuala mbalimbali ikiwemo kwa wanawake kuanzisha vikundi mbalimbali ambapo wameshajihishana pamoja na mtu mmoja mmoja amekuwa akifanya biashara zake kwa ukamilifu.



Hivyo, alisema wataendelea kumuunga mkono katika utendaji wake wa kazi na wananchi wapo pamoja nae na kuwasisitiza wananchi kuendelea kudumisha amani ya nchi iliyokuwepo.



Nae, Fatma Hassan Khamis, mkaazi wa kizimkazi, alisema kabla ya uongozi wake wa urais alikuwa akifanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu kwani alianzisha vikundi na kuviimarisha hadi hivi sasa vimekuwa vikiendelea.



Aidha alisema, kupitia tamasha hilo, pia wamepata bodi, skuli kukarabatiwa, vyumba vya kufanyia mitihani pamoja na kituo cha afya.



Hivyo, waliahidi kuendelea kumuunga mkono katika utendaji wa kazi na sasa wamekuwa wakitambulikana katika taifa kwani mgeni yoyote amekuwa akitafuta kizimkazi.



Sambamba na hayo, alisema katika uongozi wake wamekuwa wakifaidia watu wote na dhamira na nia yake ni kuendeleza kijiji hadi kijiji na masuala mbalimbali wamekuwa wakipatiwa maendeleo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI