VIONGOZI wa Chama na Serikali wamehimizwa kujenga mahusiano mazuri ili waweze kusaidia kusukuma utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Serikali badala ya wao kuwa sehemu ya kulalamika.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Tanga Rajabu Abdurahman alipokuwa akikagua mradi wa jengo la kituo cha afya Misalai kilichopo kata ya Misalai Wilayani Muheza Mkoani Tanga.
Mwenyekiti katika ziara hiyo ambayo ni mwendelezo wa ziara yake Mkoani Tanga alipata fursa ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ya huduma za kijamii kama afya,elimu,maji,miundombinu ya barabara na ujenzi wa ofisi ndogo ya CCM Kata ya Kumba.
Mwenyekiti huyo alisema Chama kitakapokuwa mstari wa mbele kufuatilia miradi ya maendeleo na kuwa na masiliano mazuri na viongozi upande wa Serikali kutawasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi katika maeneo yao kutatuliwa kero zao na kupatiwa majibu ya sababu zinazopelekea miradi hiyo kusimama.
Alisema lazima viongozi wa Chama wakiri madhaifu hayo ya kutokiwa na mawasiliano na sio jambo zuri wananchi wanapolala mika juu ya ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali na wao wawe sehemu ya malalamiko hayo.
"Haiwezekani wananchi walalamike na sisi kama chama tulalamike wakati sisi ndio tunaotakiwa kutoa majibu na njia za utatuzi wa kero kwa wananchi na si vinginevyo"Alisema Mwenyekiti huyo.
Rajabu alifafanua zaidi na kusema viongozi wa Chama wanao wajibu wa kukaa kama chama na kujadili kila aina ya changamoto zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi na kuzifiikisha katika Ofisi za Serikali ili ziweze kutafutiwa njia sahihi za utatuzi wake.
"Nilichokiona haya maalalamiko ya wananchi dhidi ya watendaji wa Serikali ni kutokana na kukosa majawabu ya kero zao laiti kama wangekuwa wanapatiwa majibu na watendaji wetu au viongozi wa chama yasingetokea haya"Alisema Rajabu.
Aidha alisema lengo la Chama chochote cha siasa pamoja na chama cha Mapinduzi ni kuunda Serikali na kuisimamia na ndio sababu ya kutembea na watumishi wa Serikali toka idarabtofauti ili waweze kutoa majawabu ya maswali ya wananchi.
Alisema hayo ndio maelekezo ya Mh,Rais aliyoyatoa kwa viongozi wa Chama kuwahakikisha kwamba wanapita katika maeneo yote na kuangalia kero za wananchi na kuzitafutia majawabu.
"Dk Samia amekuja kuwa mtu wa kutoa majawabu katika yale maeneo ambayo majawabu yalikosekana kwa muda mrefu"Alisema
Kwa upande wake Katibu Tawala Wilayani Muheza(DAS) Mohammed Mfaki alikiri kuwa Chama cha Mapinduzi kipo na kinawajibu wa kutatua kero za wananchi na kuisimamia Serikali na imetoa maelekezo ya uwajibikaji.
Aidha alisema kinyume na maagizo hayo dhahiri kutapelekea kukigombanisha Chama hicho na wananchi wake jambo haliko sawa na halitopewa nafasi katika Halmashauri ya Wilaya ya Muheza.
"Tupo pamoja na Mwenyekiti katika ziara yake ili tushirikiane nae wakati wa kutoa majibubtoka kwa wananchi juu ya kero zao ambazo zipo kwa muda mrefu"Alisema Mfaki.







0 Comments