Header Ads Widget

HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA KUWALIPA WAZABUNI WANAOINGIA MIKATABA YA KAZI KWA KIPINDI KISICHOZIDI SIKU SABA

NA AMINA SAIDI, MATUKIO DAIMAAPP TANGA 

Uongozi wa Halmashauri  ya Jiji la Tanga umeziagiza idara zake  kwamba  zihakikishe  utaratibu mzuri  wa  kuwalipa wakandarasi  wanaoingia  mikataba ya kazi katika kipindi kisichozidi siku saba tangu kuhakikiwa kazi hizo , Agizo hilo linakuja baada ya kudhihirika ucheleweshwaji unaofanywa na wakuu hao wa idara  mbalimbali  za  Halmashauri  hiyo.


Idara zinazohusika zaidi ni pamoja na Ujenzi,  Manunuzi na `Utawala,Katika kikao cha Baraza la Madiwani  kilichofanyika jijini hapa jana na leo chini ya Mstahiki Meya, Abrahaman Shiloo,  madiwani wengi walieleza kusikitishwa kwao na ucheweshwaji wa malipo kwa makandarasi wanaochukua tenda za kazi katika Halmashauri hiyo.



Walisema kuwa kitendo cha kucheleshwa kutoa malipo kwa makandarasi baada ya kukamilisha kazi zao kumesababisha  Halmashauri ya Jiji kukimbiwa na mafundi wanaotekeleza miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule za msingi, sekondari na zahanati.


Madiwani wengi walisema kuwa tenda za kazi za ujenzi  ikiwa ni pamoja na matundu ya vyoo zinakabiliwa  na changamoto  kwa  wakandarasi kutokana na kucheleweshewa malipo, Walidai kuwa ucheleweshwaji  huo wa malipo unawafanya mafundi kukimbia tenda hizo.


Diwani  wa  Mzizima,Fredick  Chiluba walisema  kuwa mafundi waliojenga matundu ya vyoo katika shule za kata yao bado hawajalipwa malipo yao ingawa walimaliza muda mrefu uliopita.


Diwani wa Pongwe, Mbaraka Sadi alisema kwamba kazi ya ukarabati wa stendi ya Pongwe haijakamilika na kwamba majibu anayopata kutoka kwa Mhandisi anayejenga stendi hiyo yanakatisha tamaa  baada ya kuletwa mchanga tripu moja tu.


Maelezo hayo ya Diwani Sadi yalizusha malumbano makali kati yake na Mhandisi wa Halmashauri ya Jiji,  Mhandisi Issa Mchezo  kuhusu idadi ya tripu,  ambaye alikanusha kupeleka tripu moja tu ya mchanga bali tripu nne.


Mstahiki Meya alilazimika kutafuta ukweli katika kauli hiyo ya idadi ya tripu za mchanga kutoka kwa Diwani Sadi na Mhandisi Issa Mchezo,  ndipo aliposimamishwa Mtendaji wa Kata ya Pongwe aeleze ni tripu ngapi za mchanga zilizoletwa katika stendi ya Pongwe.  


Mtendaji wa Kata ya Pongwe, Erika Fabian alikieleza kikao kwamba ni tripu moja tu ya mchanga ndiyo iliyoletwa katika stendi ya Pongwe.


Kutokana na maelezo ya madiwani kuhusu kuchelewa kulipwa makandarasi  malipo yao bila sababu za msingi, ndipo Mstahiki Meya baada ya kushauriana na madiwani, ikaamuliwa mkandarasi anapomaliza kazi aliyopewa na kisha kukaguliwa, anastahili alipwe malipo yake mara moja.


Akifunga kikao hicho, Mstahiki Meya aliwataka. watumishi kuwa waaminifu katika kazi zao .  Alisema uadilifu ni msingi mkubwa wa maendeleo katika nchi,

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI