Header Ads Widget

UVCCM MOSHI VIJIJINI YATIA TIMU UCHAGUZI MDOGO OLD MOSHI MAGHARIBI..

 Na Gift Mongi MATUKIODAIMA APP MOSHI.

Chama cha mpainduzi (CCM)wilaya ya Moshi Vijijini kipo katika kampeni za uchaguzi mdogo katika kata ya Old Moshi Magharibi kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo Menyasumba Macha kufariki dunia may 2023.

Tayari makada mbali mbali wa chama hicho wamepiga kambi katika kata hiyo lengo likiwa ni kutafuta ushindi wa kishindo na kuweza kuirudisha kata hiyo ndani ya mikono ya CCM.

Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Moshi Vijijini Yuvenail Shirima ni miongoni mwa makada ambao tayari wapo katika eneo hilo lengo likiwa ni kuusaka ushindi.


'Hatuchoki na hatuboi lengo ni kuhakikisha ushindi wa kishindo katika hii kata yetu ambayo ni lazima irudi katika himaya kama ilivyokuwa mwanzoni kabla ya kifo cha Macha'anasema Shirima


Kwa mujibu wa Shirima ni kuwa hakuna kazi ndogo mathalani linapokuwa suala la uchaguzi na kuwa ni lazima kutumia njia sahihi katika kuusaka ushindi.

'Huwezi ukalala ndani ukategemea ushindi na ndio maana tupo hapa kuzisaka hizi kura ila hao wengine wabaki na lawama zao baada ya matokeo watajua hawajui'anasema

Gerson Onesmo mkazi wa Old Moshi anasema kuwa kampeni zinazoendeshwa na CCM zimekuwa za kistaarabu na kuwa ni ukomavu wa siasa na wananchi kwa sasa hawataki porojo wanataka maendeleo.

'Tunaenda kuendelea pale tulipoishia na sasa niwahakikishie kata yetu inaenda kurudi katika mikono salama'anasema


Menyasumba Macha alikuwa diwani wa tatu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro kupoteza maisha na kufanya idadi ya kata zilizoko wazi kufikia tatu, kata hizo ni pamoja na Old Moshi Magharibi (Moshi), Kalimawe na Njoro (Same).


MWISHO.





 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI