Na Mwandishi Wetu, Mtwara
Meneja wa Uendelezaji na Uzalisha wa Gesi wa shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania Felix Nanguka amesema kuwa shirika hilo limekuja na mpango kabambe wa kuhakikisha kuwa wanaongeza kiwango cha uzalishaji wa gesi nchini hadi kufikia futi za ujazo milioni 17 toka futi za ujazo milioni10.
Ametoa kauli hiyo jana Msimbati Mnazibay ambapo amesema kuwa ili kuhakikisha zoezi hilo linakamilika TPDC kwakushirikiana kampuni ya Mourel & Prom wanafanya uboreshaji katika miundombinu kwakutumia mafundi wa ndani na nje ya nchi.
“Hili ni zoezi mahususi ambalo linaashiria kuwa sasa tumeaanza ukarabati wa visima vyetu vya eneo hili ambavyo viko vitano”
“Baada ya uboreshaji tutaangalia sasa na vituru vingine kwaajili ya uendelezaji ambapo mpaka sasa tuna visima 104 huku visima 38 vikiwa vimechimbwa vimechimbwa baharini tunaimani kuwa vitakuwa na mchango mkubwa hasa ukizingatia kuwa tuna kiwanda cha LNG lakiini pia ni nishati muhimu ambayo tunatumia kuzalishia umeme nchini”
Aidha Msimamizi Mkuu wa Uzalishaji Maurel & Prom Hussein Chitemo amesema maboresho hayo makubwa yataongeza kiwango cha gesi.
“Wakati wa maboresho tunaingiza vifaa maalum kwenye visima vya gesi ambavyo vitasaidia sisi kuongeza uzalishaji zaidi ya futi za ujazo milioni 7 hivyo kuwa na futi za ujazo milioni 17 wakati wa maandalizi yalichukua muda mrefu sana lakini baada ya kukamilika tutamaliza kazi kwa siku nne tu” alisema Chitemo
0 Comments