Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP, NJOMBE,
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru mkoa wa Njombe imesema Kusuasua kwa utekelezaji wa miradi ya serikali ukiwemo ujenzi wa madarasa kupitia fedha za Boost kunakwamisha malengo yaliyowekwa ya kuhakikisha ujenzi unakamilika ndani ya siku 90.
Mbele ya vyombo vya habari wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu kwa kipindi cha miezi mitatu Kamanda wa Takukuru mkoa wa Njombe Ephreim Cassim amesema wamebaini kuwapo kwa miradi 7 ya boost yenye tahamani ya shilingi bilioni 14.6 inayotekelezwa kwa kusua sua ilihali wahandisi wapo.
Kutokana na changamoto hizo Kamanda Cassim Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama au kwa viongozi waliopo karibu nao pindi wanapobaini ubabaishaji wowote katika miradi ya serikali.
Kwa upande wao wananchi mkoani Njombe akiwemo Andrea Mselela na Simon Mligo wametaka kuchukuliwa hatua kwa watendaji wanaokwamisha jitihada za serikali katika kutekeleza miradi yao.
Pamoja na mambo mengeni Takukuru imesema inaendelea kuchunguza miradi mbalimbali inayotekelezwa ukiwemo ule wa shule mpya ya mkoa wa Njombe ya wasichana inayojengwa katika kijiji cha Usalule wilayani Wanging'ombe ambayo imebainika kutekelezwa kwa kusuasua kinyume na mkataba.









0 Comments