Header Ads Widget

PONDEZA AMEPONGEZA TIMU ZILIZOINGIA FAINAL NA KUSHANGAA MUITIKIO WA MASHABIKI

NA MATUKIO DAIMA APP,ZANZIBAR

MBUNGE wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza amezipongeza Timu zilizoingia Fainali katika Mashindano ya Maalum ya Pondeza Chumbuni Festival ambayo yanalengo la kudumisha Umoja na kuibua vipaji vya Vijana katika Jimbo hilo.


Timu zilizoingia fainali katika Tamasha la Pondeza Chumbini Festavali ni ppamoja na  Mwembe Makumbi na  Karakana ambapo fainali inatarajiwa kuchezwa Mwishoni wikii.


Akizungumza na Waandshi wa Habari mara baada ya kumalizika kwa Mchezo wa Fainali Mbunge wa Jimbo hilo Ussi Salum Pondeza amesema kuwa, anazipongeza Timu ambazo zimefika katika hatua ya fainali ambapo anawatakia maandalizi mema kuelekea mchezo huo.


Aidha Mbunge  huyo ameeleza hali halisi ya Mashindano hayo kuelekea kilele na kuwapongeza Wananchi kwa namna walivyoshaijihishika na kujitokeza kwa Wingi katika Mashindano hayo.


"Kiukweli Mashaindano yalikuwa Mazuri hivyo niwapongeze Timu zote ambazo zimeingia Fainali sasa kikubwa kutoka kwao wajiandae na Mchez huo kwani kutakuwa na zawadi kubwa ambayo inaendana na hadhi ya Mashindano," amesema.


Amefafanua kuwa, Kamati ya Mashindano imepokea Mapendekezo mbalimbali kuhusu kiwanja cha Kilele cha Mashindano pamoja na kuongezwakwa baadhi ya Michezo.


"Ukweli kuwa Mashindano yamekuwa na Mvuto mkubwa na kuitikiwa na Watu wengi hivyo kamati ya Mashindano imepokea mapendekezo ya kubadili Uwanja pamoja na kuongeza Baadhi ya Michezo," amesema.


Hata hivyo amesema Siku ya Kilele kutakuwa na Michezo mbalimbali huku kukiwa na burudani kutoka kwa Wasanii wa Kizazi kipya kutoka Bara na Zanzibar.


Ameongeza kuwa, Tamasha hilo ambalo limebeba jina la Pondeza Chumbuni Ferstival litakuwa muendelezo kwa michezo mbalimbali ambapo washindi watakabidhiwa Fedha Taslim.


Mapema, Mchezaji wa Timu ya Chumbuni Seif Juma amepongeza Timu yake kwa kuibuka na Ushindi na kuhaidi kujipanga vyema katika Mchezo wa Fainali.


"Kwa sasa tunajipanga vyema kuelekea Mchezo wa Fainali na kuibuka na Bingwa katika Mashindano haya," Amesema.


Nae, Mchezaji wa Chumbuni Rashid Juma amepongeza wapinzani wao kwa kuibuka na Ushindi katika Mchezo huo huku akiahid kujipanga mchezo wa Mshindi wa Tatu.


Pondeza Festival imeandaliwa na Taasisi ya Pondeza Foundation ikiwa na lengo la kuwaunganisha Wananchi katika Jimbo la Chumbuni ambapo Kielele cha Mashindano hayo kinatarajiwa kufanyika Siku ya Jumapili Wiki hii.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI