Mjumbe wa Halmashauri Mkuu ya CCM taifa M - NEC Hamoud Jumaa amewataka viongozi wa CCM na wanaCCM kwa ujumla kuhakikisha wanaongeza wanachama katika Chama Cha Mapinduzi kwaajili ya kuhimalisha uhai wa Chama kipate ushindi ili kushika dola.
Amesema hayo mjini Kibaha mkoani Pwani wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara wa majumuisho ya ziara ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha Mwajuma Nyamka ambapo alikuwa Mgeni rasmi.
Amesema jitahidi kadri ya uwezo wenu na tufanye kazi ya kutosha kuhakikisha mnaongeza wanachama wa CCM ili wawe wengi maana nguzo ya msingi duniani ni kukamata dola na huwezi kukamata dola bila ya kuwa na wanachama wakutosha.
"Nataka niwaambie ndugu zangu Chama lazima kihimalike na tuna misingi yetu ya Chama katika katika yetu kwenye ibala ya tano inazungumzia namna ya kushika dola na vyama vyote duniani nguzo yake ya msingi ni kukamata dola lazima tuongeze wanachama" amesema Jumaa.
Ameongeza kuwa tuhakikishe tunaongeza wanachama na kuhakikisha wanachama hao wanakuwa hai kwa kulipa ada za kila mwezi sambamba na kuwalinda sana wanachama wetu.
Aidha akizungumzia kupelekea chaguzi za serikali za mitaa mwakani Jumaa amesema ni wakati wa wanachama wa chama hicho kushikamana na kujiandaa kushinda kwa kishindo chaguzi zijazo.
Amesema kwamba wanachama wanatakiwa kushikamana ili waweze kupata ushindi wa kishindo katika chaguzi zijazo huku akisisitiza utoaji wa ada.
Ameyaeleza hayo katika mkutano wa majumuisho ya ziara ya Mwenyekiti wa CCM Kibaha mjini ambao ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho.
Aidha amesema wadau wanaojitolea kusaidia chama waruhusiwe kwa kufuata taratibu na kanuni za chama hicho.
Jumaa amesema wanaojitokeza kuchangia chama hawatakiwi kuziwa badala yake wazingatie taratibu na kufuata kanuni na kwa kufanya hivyo itaondoa migogoro kwenye chama.
" Msiwazuie watu kuchangia lakini utaratibu ufuatwe, chama kinaruhusu wadau kuchangia kwa kufuata taratibu hata baadae ukitaka kugombea utaulizwa umekifanyia nini chama kwahiyo kwenye chama lazima ujitolee" amesema.
Amesema Mbunge aliyepo madarakani anatakiwa kupewa nafasi afanye kazi yake akitekeleza Ilani ya Chama na wachangiaji waendelee kwa kufuata kanuni.
Jumaa ametumia nafasi hiyo kumpongeza mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka kwa kufanyakazi vizuri huku akimtaka aendelee kuchapakazi kwa ajili ya kutekeleza ilani ya uchaguzi kwakuwa CCM imeingia mkataba na wananchi na lazima isimamiwe vizuri
Mwenyekiti wa CCM Kibaha Mjini Mwajuma Nyamka amesema chama hicho hakiwezi kujengwa na mtu mmoja hivyo wadau wanaojitokeza kuchangia wazingatie kufuata taratibu na kanuni.
Nyamka amesema miradi ya maendeleo imetekelezeka kwa asilimia 90 na vikwazo kwa wananchi vimepungua huku akisisitiza Mbunge wa Jimbo hilo Sylvestry Koka aachwe afanye kazi ya kutekeleza Ilani katika kipindi ambacho yupo madarakani.
Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani David Mramba amesisitiza umoja kwa wanachama ili kukiwezesha chama hicho kushinda kwenye chaguzi zijazo.
Nae mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka,amewashukuru wanachama, mabalozi wa mashina, wenyeviti kuendelea kushirikiana ili kukiimarisha Chama.
Koka amesema kuwa kwa kushirikiana na serikali na wananchi wameendelea kukabili changamoto kwenye jimbo hilo.
+++++++++
0 Comments