Header Ads Widget

MWAKYOKOLA NA UGUNDUZI WA BAJAJI YA SOLA


Na Johnson Jumanne-Matukio App, Mbeya.

Huku bei ya mafuta ikizidi kuwa changamoto nchini Tanzania na wananchi wakizidi kulalama kila siku kutokana upandaji bei wa mafuta, hali hii imekuwa tofauti mkoani Mbeya ambako Maonesho ya Nanenane yamezinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamuhuli Wa Muungano wa Tanzania Mh. Philip Mpango kwa ajili ya kuanza rasmi kwa maonesho hayo ambayo ilikuwa ni siku ya jana.


Kutokana na changamoto ya mafuta kuwa bei juu karibu kila sehemu nchini Tanzania jijini Mbeya kijana ajulikanaye kwa jina la Joel Japhet Mwakyokola ameweza kuwa tofauti baada ya kuja na mbinu tofauti ya janga hilo baada kuweza kugundua bajaji inayotumia umeme wa jua au sola kwa ajili ya kpunguza changamoto hiyo ya mafuta.

Japhet mwakyokola anasema “niliwaza kwanini tusitumie mbinu mbadala kwamba mtu anaweza akatumia mafuta kama hakuna jua pia akatumia umeme wa sola kama kuna jua kwasababu mwenyezi Mungu ametubaliki kiwango kikubwa cha jua hivyo atuwezi kukipoteza bure hususani kwa Maisha ya Mtanzania naona hii itakuwa mbinu mbadala kwa Maisha ya watanzania.


Pia Joel anaamini kwamba akiwaza kufanikisha ndoto yake hiyo basi ataweza kurahisisha gharama za usafiri nchini Tanzania na kuweza kutatua shida ya usafiri ambayo imekuwa changamoto katika kila eneo na hivyo kurahisisha kwakupunguza gharama hizo za mafuta.


Maonesho haya ya ni muendelezo wa maonesho ya nanenane ambayo hufanyika kila mwaka nchini Tanzania na lengo lake kuu ikiwa ni kuinua Sekta kilimo nchini Tanzania kutokana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI