NA HADIJA OMARY_ LINDI.....
Tume ya taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Liwale Mkoani Lindi imeanza kuwezesha uandaaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji 6 ili kudhibiti muingiliano baina ya shughuli za kibinadamu na wanyama Katika maeneo yanayopakana na hifadhi ya taifa ya Nyerere
Hayo yameelezwa na Afisa ardhi Mwandamizi kutoka tume ya taifa ya mipango ya matumizi ya ardhi Ortumar Komba akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa mradi huo mbele ya mkuu wa wilaya ya Liwale amesema mradi huo utahusisha upimaji wa vijiji, kuandaa vyeti vya vijiji , kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi pamoja na kutayarisha hati za kimila
Aidha amesema Mradi huo umewezeshwa Kwa Ushirikiano wa Halmashauri ya wilaya ya Liwale, hifadhi ya taifa ya Nyerere, Frankfurt Zoological Society, TANAPA pamoja na Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Lindi
Goodluck Mlinga ni Mkuu wa wilaya ya Liwale amesema hatua ya kuanza utekelezaji wa upimaji wa matumizi ya ardhi kwa wilaya ya Liwale itasaidia kuleta amani na utulivu ikiwemo kuondoa migogoro hasa ya wakulima na wafugaji sambamba na changamoto ya uvamizi wa wanyama waharibu hususan Tembo
Vijiji vitakavyonufaika na Mradi huo ni pamoja na Ndunyungu, Mpengere, Ngorongopa, Mitawa, Lubaba na Nambinda
0 Comments