Na Gift Mongi MATUKIO DAIMA APP MOSHI
Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi ameendelea na ziara ya kutembelea jimbo lake la Moshi Vijijini kwa kutembelea Kata ya Kimochi.
Ziara hiyo ilianza kwa kutembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa katika Kata ya Kimochi.
Mbunge aliambatana na Katibu wa CCM Wilaya ya Moshi Vijijini Ndugu Ramadhani Mahanyu, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Andrew Mwandu, Madiwani wa Viti Maalum kutoka Tarafa za Hai Mashariki na Kibosho, viongozi wa CCM Kata na Matawi kutoka Kimochi na Watendaji wa idara mbalimbali toka Serikalini.
Prof Ndakidemi alianza ziar
Ofisi ya Kijiji cha Mdawi ambapo ujenzi huo unaendelea kwa nguvu za wananchi. Katika ujenzi huo Mhe Mbunge aliwahi kuchangia kiasi cha shilingi milioni moja ili kuunga mkono juhudi za
Wananchi.
Mbunge na viongozi wengine alioambatana nao waliendelea na ziara kwa kukaguaa mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi ya Tarafa ya Hai Mashariki katika kijiji cha Shia ambapo Serikali imetoa shilingi milioni 90.
Timu iliyoambatana na Mbunge iliridhishwa sana na kazi ya ujenzi inayoendelea. Kazi ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ilikamilka kwa kutembelea ukarabati wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari ya Komakya ambapo alichangia shilingi laki tano ili zisaidie kutatua changamoto ya kuingiza
Mbunge alihimiza kazi ikamilike haraka na wanafunzi waanze kupata huduma ya bweni. Akiwa katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kisaseni, Wananchi waliowasilisha kero zao kwa Mbunge kwa nyakati tofauti wamesema kuwa ushirikishwaji wa wananchi katika miradi ya maendeleo inayoletwa na Serikali katika Kata yao kama ile ya barabara kumekuwa na sintofahamu.
Walisema, hawapewi taarifa za thamani ya miradi inayoendelea katika kata yao, na wakapendekeza viongozi wao wa vijiji na vitongoji washirikishwe katika hatua zote za utekelezaji wa miradi. Wananchi wengi waliochangia katika mkutano huo walionyeshwa kukerwa na ubovu wa barabara katika Kata ya Kimochi na ujenzi ulio chini ya kiwango.
Baadhi walionyesha uhitaji wa kujengewa barabara kwa kiwango lami. Kero ingine iliyowakilishwa kwa Mbunge ni kukosekana kwa shule ya Sekondari katika ukanda ya milimani ambapo watoto hutembea umbali wa kilomita 28 kwenda kupata elimu katika shule ya Sekondari Komakya.
Ili kukabiliana na changamoto hiyo, wananchi wameiomba Serikali iruhusu baadhi ya majengo ya shule ya Msingi Kisaseni yatumike kuanzisha shule ya Sekondari kwani kuna madarasa, ofisi na matundu ya choo ambavyo havitumiki kwa sasa.
Akina mama waliokuwa kwenye mkutano walimwomba Mbunge awasaidie kuwasilisha kero wanayokumbana nayo ya kunyimwa fursa ya kukata majani na kuokota kuni kwenye eneo la half mile kwenye mpaka wa vijiji na mlima
Kilimanjaro.
Kero nyingine zilizoibuliwa kwenye mkutano huo ni uharibifu unaofanywa na Tumbili na Kima, na kukosekana kwa mitaji ya kujiendeleza kwa vijana. Akijibu
hoja za wananchi, Mbunge aliwaahidi kuwa kero zote zilizoibuliwa katika mkutano wake atazipeleka katika mamlaka mbalimbali serikalini ili zipate ufumbuzi.
Mwisho.
0 Comments