Header Ads Widget

MARUFUKU KUONGEZA HATA SHILINGI MKULIMA KUPATA SALFA.


Na Scola Ramadhani - Matukio Daima App, Mkuranga.

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nasri Ally amepiga malufuku kuongeza kiasi chochote cha fedha kwenye Viwatilifu aina ya Salfa vya zao la korosho vilivyosambazwa Wilaya humo na serikali kwa Wakulima Wilayani humo.


Amesema hayo mjini Mkuranga wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Mkuranga amesema Viwatilifu hivyo hutolewa bure kwani ni ruzuku kutoka serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kumsaidia mkulima wa korosho Wilayani anufaike na kilimo chake.


Amesema "Hatutaki Mheshimiwa Rais agombanishwe na Wananchi wa Wilaya ya Mkuranga alitafuta fedha na akahakikisha Salfa inakuja bure isiongezwe ziada Wala isiongezwe gharama ambayo haikuelekezwa"

"Kwahiyo naomba tukayasimamie hayo katika Kata zetu na mkawaeleze Wakulima Salfa hiyo ni haki yao kuipata bila kutoa hata senti moja maana hayo ndio maelekezo kutoka kwa Mheshimiwa Rais"


Akizungumza kwa Njia ya simu Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushirika wa Wakulima mkoa wa Pwani CORECU Musa Mng'eresa amesema kulikuwa na vyama vya msingi - Amcos vitatu vya Kata ya Magawa Wilayani Mkuranga likuwa vikiwatoza gharama za usafiri Wakulima wakati wa kuchukua Salfa zao lakini baada ya CORECU kufuatilia na baada ya kupewa maelekezo wakaacha.


"Sisi CORECU kama Ushirika tulipeleka Salfa hizo hadi kwenye vyama vyote vya msingi mkoani Pwani lakini wale Viongozi wa vyama walikuwa wanafanya huo ubadhirifu kwa kuwaambia Wakulima wachangie kwa mfuko Kati ya shilingi 1000/- na shilingi 1500/-"


"Mimi nasisitiza hizo dawa zimekuja za bure zimetolewa na serikali na sisi CORECU tumewasambazia Wananchi kama inavyotakiwa kwahiyo ni malufuku Chama chochote cha msingi kumchaji mkulima yeyote kiasi chochote kuhusu hiyo pembejeo" amesema Mng'eresa.

Ameongeza kuwa "anayechukua hizo pembejeo awe na shamba tutakuja kuhoji Salfa ulizochukua umepeleka wapi asipokuwa na chakuonyesha alikopeleka Salfa hatua kali za kisheria zikichukuliwa dhidi yake" 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI