BODI ya wakurugenzi ya wakala wa Maji na Usafi wa mazingira Vijijini (RUWASA) imemtaka Mkandarasi wa Mradi wa Maji Malangali-Hanjawanu (Igando-Kijombe) kampuni ya STC ya Dar es Salaam kukamilisha kazi ndani ya miezi miwili ya mkataba iliyobaki.
Akichangia Leo wakati wa ziara ya bodi hiyo iliyoongozwa na mwenyekiti wake Mhandisi Ruth Koya , mjumbe wa Bodi hiyo Mhandisi Mpembe amesema, wananchi waandaliwe ili kuupokea mradi wao.
Pia wameataka wananchi kutunza mazingira pamoja na mradi ili uweze kuwahudumia kwa muda mrefu.
Kwa upande wake mjumbe kutoka Bodi hiyo anaeiwakilisha Wizara amesema maandalizi ya uzinduzi wa mradi yanaendelea kwakuwa miezi miwili ni kidogo sana.
Bodi ya RUWASA inaendelea na ziara ya ukaguzi wa miradi ya mqji vijijini kujionea utekelezaji wa miradi sambamba na utoaji wa huduma ya maji vijijini.
0 Comments