NA WILLIUM PAUL, ROMBO.
CHAMA Cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro kimezindua kampeni za marudio ya uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Marangu kitowo wilayani Rombo jana na kumnadi mgombea wake Simon Massawe.
Akizindua kampeni hizo Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi amesema kuwa, Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hasani imefanya maendeleo makubwa katika wilaya ya Rombo na mkoa wa Kilimanjaro.
Boisafi amesema kuwa, wananchi wanawajibu wa kulipa kutoka na kazi hizo ambapo malipo yake ni kumchagua mgombea udiwani anayetokana na CCM, Simon Massawe katika uchaguzi utakaofanyika Septemba 19 mwaka huu.
Amesema kuwa, mwaka 2020 Chama cha Mapinduzi kilipita na kunadi Ilani yake na kuomba kura ambapo wanachi waliielewa na kuwachagua Madiwani, Wabunge na Rais wanaotokana na chama hicho ambapo kimetekeleza Ilani hiyo kwa vitendo.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa, tangu kuingia kwa awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hasani imepita miaka miwili ambapo kazi kubwa zimefanyika na zinaonekana zikiwa na malengo ya kuwaletea wananchi maendeleo.
"Wananchi wa Marangu kitowo hakuna zawadi mnayoweza kumlipa Rais Dkt Samia Suluhu Hasani kutokana na kazi anazozifanya katika kati hii na wilaya kwa ujumla zaidi ya kumpa kura za kishindo mgombea anayetokana na Chama chake ambaye ni Simon Massawe" anasema Boisafi.
Mwenyekiti huyo pia alitumia nafasi hiyo kuwataka wanachama wa Chama cha Mapinduzi kuhakikisha miradi inayotekeleza katika maeneo yao inazingatia ubora na thamani ya fedha.
"Wanaccm mnawajibu wa kuhakikisha mnaisimamia na kukagua miradi mbalimbali inayoletwa katika maeneo yenu na pale mnapoona haiendi sawa ama kunaufujaji wa fedha toeni taarifa mapema ili hatua ziweze kuchukuliwa haraka kabla ya mradi kujengwa chini ya kiwango"
Naye Katibu wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro, Jonathan Mabihya alisema kuwa, Serikali kwa sasa inaongozwa na chama cha Mapinduzi na kuwataka kutofanya makosa kwa kuwachagua wagombea ambao hawatokani na chama hicho.
"Wananchi mnawajibu wa kuchagua je mnachagua maendeleo au mnachagua kurudisha nyuma maendeleo mchagueni Simon yeye anaongea lugha moja na Serikali ili aweze kumalizia zile kazi zilizokuwa zimeanzwa na mtangulizi wake"
Katibu huyo alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wa Marangu kitowo kukikopesha imani chama cha Mapinduzi ili kiweze kuwalipa maendeleo na kufanya hivyo hawatajutia maamuzi yao.
Kwa upande wake, Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro, Abraham Urio alisema kuwa kunakuchagua Diwani na Diwani mwakilishi wa wananchi na kudai kuwa Simon atakuwa Diwani mwakilishi wa wananchi na kuwapambania kuwaletea maendeleo pamoja na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili.
Naye Mgombea, Simon Massawe aliahidi endapo akichaguliwa atahakikisha matatizo yanayowakabili wananchi wa Marangu kitowo yanapatiwa ufumbuzi katika kipindi chake cha uongozi.
0 Comments