Header Ads Widget

KAZI YAENDELEA MOSHI VIJIJINI...

 Na Gift Mongi MATUKIO DAIMA APP 

 Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi   ameendelea na  ziara ya kutembelea Jimbo lake la Moshi Vijijini kwa kutembelea kijiji cha Mandaka Mnono kilichoko ukanda wa chini katika Kata ya Oldmoshi Magharibi.

Ziara hiyo ilianza kwa kutembelea vikundi viwili vya wekeza (Shine na Baraka Groups), zahanati ya kijiji cha Mandaka Mnono, korongo la Manguvu na eneo kutakakojengwa Skimu ya Umwagiliaji ya Mandaka Mnonono




Aidha Prof Ndakidemi aliambatana na Katibu wa Wazazi Wilaya ya Moshi Vijijini Comrade Andrew Mwandu, Madiwani wa Viti Maalum kutoka Tarafa za Hai Mashariki na Kibosho, viongozi wa CCM Kata na Matawi kutoka Oldmoshi Magharibi na Watendaji wa idara mbalimbali toka Serikalini.

Mbunge alianza ziara kwa kujionea shughuli za kikundi cha Shine ambao wamejiunga kwa malengo ya kufuga mbuzi, kulima mpunga na kufanya biashara ndogo ndogo. Wakisoma risala, walimweleza Mbunge kuwa wamepiga hatua kubwa, na wana nia ya kununua mashine ya kusaga, ila mtaji wao ni kidogo. Mbunge aliahidi kuwachangia shilingi milioni moja.


 Alipotembelea kikundi cha wekeza cha Baraka, Mbunge aliwapa moyo na kuwashauri waendelee kujipanga vizuri ili akirudi tena aangalie namna ya kuwasaidia kuongeza mtaji wao. Alipotembelea zahanati ya Mandaka Mnono, pia  alielezwa kuwa wana changamoto ya maji ya kunywa na uhaba wa watumishi. 

Mbunge na ujumbe wake walitembelea korongo la John Manguvu ambapo walipokea kero ya kutokuwepo kivuko cha kuunganisha vitongoji vya Saningo, Mnono Kati na Uswahilini.

 Vilevile, Mbunge alitembelea bonde la Mandaka Mnono ambalo limepatiwa mradi wa Skimu ya Umwagiliaji ili kuendeleza kilimo cha mpunga.

Akiwa katika mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Mnono Kati, Mbunge aliwaeleza wananchi juhudi kubwa zilizofanywa na serikali kuwaletea maendeleo katika sekta za elimu, kilimo, miundombinu ya barabara, umeme, maji na maendeleo ya jamii ambapo zaidi ya shilingi Bilioni  5.5 zimeshaelekezwa katika miradi hiyo ya maendeleo.



 Katika mkutano huo, wananchi wakiwasilisha kero zao ikiwemo
 ya ubovu wa barabara na ya maji safi ya kunywa  ziliibuliwa na wananchi wengi waliopata nafasi ya kuongea. 

Kero ingine kubwa iliyolalamikiwa ni kukosekana kivuko katika
Korongo la Kwa Saning'o. Wananchi walieleza kuwa hivi sasa korongo hilo halina kivuko na wakati wa mvua na mafuriko wanafunzi hushindwa kwenda shule jirani katika kata ya Mabogini pamoja na adha kubwa wanayoipata mama wajawazito kuja zahanati ya Mnono.

Kero nyigine iliyoibuliwa ni ombi la kijiji cha Mandaka Mnono kuwa Kata inayojitegemea. Kero nyingine ilihusiana na uharibifu wa makusudi unaofanywa na jamii ya wafugaji kwa kulisha mifugo katika mashamba ya wakulima. 

Mwisho.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI