Header Ads Widget

KARIMU MANDONGA, DULLA MBABE NA MABONDIA WENGINE ZAIDI YA 14 WATUA ZANZIBAR KWA KISHINDO

 



NA THABIT MADAI, ZANZIBAR- MATUKIO  DAIMA APP


KUELEKEA  Usiku wa Masumbwi Visiwani Zanzibar Agost 27 mwaka huu, Mabondia Karimu Mandonga, Dulla Mbabe na Mabondia wengia zaidi ya 14 wamewasili Visiwani Zanzibar  kwa ajili ya ziara maalumu na kupima uzito kulekea mapambano yao ya  masumbi katika Uwanja wa Mao Tsung Mjini Unguja.


Ziara ya Mabondia hao ilianza katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Ofisi Kuu za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui ambapo walipata fursa ya kusoma Dua katika Kaburi la Muasisi wa Mapinduzi na Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume.


Akizungumza wakati wa Mapokezi ya Mabondia hao Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Unguja Idrissa Kitwana Mustafa amesema kuwa, amefarijika kwa kutembelewa na Mabondia hao na kuhakikishia Ulinzi na Usalama kuelekea siku ya Mapambano hayo.


Nae Afisa Uhusiano wa TOSH SPORT  Matlada Peter, ujio wao Visiwani humo ni maandalizi kuelekea Mapambano hayo Agost 27 mwaka huu ambapo siku ya Kesho Mabondia wanatarajiwa kupima Afya.


Kwa upande wao  Mulla JR kutoka Zanzibar na Karimu Mandonga wameeleza namna walivyojipanga kutoa burudani kwa Mashabiki mchezo huo.



Ikumbukwe kuwa Mara ya Mwisho Zanzibar kucheza Mchezo wa Ngumi za ilikuwa Mwishoni mwa miaka ya 1960 baada ya katazo la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayyat Sheikh Abeid Aman Karume.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI